STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 9 Machi 2016

HUYU NDIE MCHEZAJI BORA WA FEBRUARY LIGI KUU BARA........


 
Mshambuliaji Mohamed Mkopi wa timu ya Tanzania Prisons amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Februari kwa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu wa 2015/2015.

Mkopi katika mwezi huo uliokuwa na raundi nne, alicheza mechi zote nne za timu yake dhidi ya Mbeya City, Yanga, Mwadui na Mgambo Shooting. Alitoa mchango mkubwa kwa timu yake katika mechi hizo ambapo zote ilitoka sare, hivyo kupata jumla ya pointi nne.

Katika mechi hizo ambapo Tanzania Prisons ilifunga mabao matatu, Mkopi alifunga bao moja na kusaidia kupatikana mabao mengine mawili.

Mshambulaiji wa Prisons ya Mbeya, Mohamed Mkopi akimtoka beki wa JKT Ruvu, George Minja wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliozikutanisha timu hizo kwenye uwanja wa Karume, Dar  Mshambulaiji wa Prisons ya Mbeya, Mohamed Mkopi akimtoka beki wa JKT Ruvu, George Minja

Mshambuliaji huyo ambaye mpaka sasa amefunga mabao sita kwenye Ligi hiyo, aling’ara zaidi katika mechi mbili kati ya hizo nne ambapo alichaguliwa kuwa mchezaji bora.

Mkopi ambaye ni mshambuliaji wa kati alichaguliwa mchezaji bora kwenye mechi dhidi ya Mwadui iliyochezwa mkoani Shinyanga, na ile dhidi ya Yanga iliyofanyika Uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.

Kwa kunyakua tuzo ya mchezaji bora kwa Februari, Mkopi atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) na wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom.

Wachezaji bora wa miezi miwili iliyopita ni kiungo Thaban Kamusoko wa Yanga (Desemba 2015), na beki Shomari Kapombe wa Azam FC (Januari 2016).

Imetolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox