Siri
ya mafanikio ya Leicester City kufanya vizuri Ligi Kuu England msimu
huu imegundulika, si nyingine bali ni baraka za Mtawa wa Kithailand!
Phra
Prommangkalachan, mtawa wa Kibudha amekuwa akitembelea maskani ya
Leicester mara kwa mara kwa takribani miaka mitatu mfululizo,
akiubariki uwanja na kuwafanya wachezaji kuwa na furaha muda wote.
Hivyo
anaamini kwamba safari zake za mara kwa mara zimekuwa na matokeo chanya
na kuleta bahati kubwa kwa timu hiyo, na kupelekea klabu kuongoza ligi
kwa pointi tano mbele ya Tottenham wanaoshikilia nafasi ya pili huku
wakisaliwa na michezo nane tu kumaliza msimu.
"Huwa
nawaning'inizia hirizi kwenye shingo zao na kuwafanya wawe na furaha
isiyo na kifani inayowapelekea kuwa na nguvu nyingi za kupambana
uwanjani," alisema.
"Sijui kama walielewa nilichowaelezea kuhusu hilo, lakini walijua kwamba nilikuwa nikiwapa bahati
Mmiliki
wa Leicester Vichai Srivaddhanaprabha inasemekana ni muumini mtiifu wa
imani ya Budha na anaamini msimu huu timu yake itatwaa ndoo ya EPL
katika uwanja wa King Power ambapo mara zote helikopta huwa inatua
hapo.
"Alimleta mtawa kwa sababu ya kuleta baraka kwa timu, uongozi na wachezaji kwa ujumla", aliongeza


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni