Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imepanda kwa nafasi moja kwenye
viwango vya Shirikisho la Soka Duniani, FIFA baada ya kujikusanyia alama
278.
Tanzania imeshikilia nafasi ya 125 duniani kwenye viwango vilivyotolewa hii leo, Machi 3, 2016.Ethiopia imeporomoka kwa nafasi sita hivyo kuifanya ishikilie nafasi ya 124 duniani huku Burundi ikishikilia nafasi ya 119 duniani baada ya kuporomoka kwa nafasi tisa.
Timu ya taifa ya Kenya imefanikiwa kupanda kwa nafasi mbili hivyo kushikilia nafasi ya 99 ulimwenguni na Rwanda, Amavubi ikishikilia nafasi ya 85 duniani baada ya kupanda kwa nafasi sita.
Uganda inaongoza kwa Afrika Mashariki licha ya kuporomoka kwa nafasi nane na kuifanya ishikilie nafasi ya 70 duniani.
Ubelgiji bado imeshikilia nafasi ya kwanza duniani huku taifa la Brazil likishikilia nafasi ya sita ulimwenguni.
Cape Verde wametua kileleni mwa orodha ya Fifa ya uchezaji kandanda barani Afrika ya mwezi Machi.
Wamefanikiwa kuwapita mabingwa wa Afrika wa mwaka 2015 Ivory Coast ambao wameshuka hadi nambari mbili.
Cameroon pia wameimarika, na kuingia katika orodha ya 10 bora na kuwaondoa Guinea.
Licha ya kushinda Kombe la Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameshuka nafasi moja hadi nambari 58.
Miongoni mwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Uganda inaongoza ikiwa nambari 67, ikifuatiwa na Rwanda (85), Kenya (103), Tanzania (125), Burundi (129) na Sudan Kusini (140).
Mataifa yanayoshika mkia Afrika n Somalia, Eritrea na Djibouti, yote yakiwa nambari 204.
Duniani, Ubelgiji wanaongoza wakifuatwa na Argentina.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni