
STORI YA KWANZA;
Bayern Munich imepambana kutoka nyuma kwa goli 2-0 hadi kuichapa Juventus kwenye dakika za nyongeza na kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali ya Champions League.
Timu hizo zilitoka sare ya kufunga kwa bao 2-2 kwenye mchezo wa kwanza, Paul Pogba na Juan Cuadrado wakaifungia Juve na kuiweka mbele kwa bao 2-0 dhidi ya Bayern kwenye mchezo wa jana usiku.
Robert Lewandowski alipiga bao kwa kichwa na kufufua matumaini ya Bayern kubadili matokeo kabla ya Juve kumruhusu Thomas Muller kusawazisha katika dakika ya mwisho na kuufanya mchezo kuwa sare ya magoli 2-2 na kulazimisha timu hizo kwenda kwenye dakika za nyongeza.
Bayern wakafuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Ulaya kwa style ya aina yake baada ya Thiago na Kingsley Coman kuifungia timu yao mabao mawili katika muda wa nyongeza. Mchezo huo ukamalizika kwa Bayern kuichapa Juve magoli 4-2 na kufanya jumla ya magoli yote ya michezo miwili kuwa Bayern 6-4 Juve.
Juve ambao walitawala mchezo kwa asilimia nyingi za muda wa kawaida
walichanganywa na goli la kusawazisha la dakika za lala salama la Muller
pamoja na mabadiliko yaliyofanywa na Guardiola ya kuwaingiza Coman na
Thiago ambao waliamua mchezo.Mbali na kupoteza mchezo huo, kinachowaumiza zaidi Juve ni goli lilifungwa na Coman mchezaji wao kinda ambaye yupo Bayern kwa mkopo wa muda mrefu.

Kijana huyo wa kifaransa mwenye miaka 19, ali-assist magoli matatu wakati Bayern inashinda bao 5-0 dhidi ya Werder Bremen kwenye mchezo wao wa ligi weekend iliyopita na alikuwa kwenye kiwango bora baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Xabi Alonso.

STORI YA PILI;

Barcelona ambao ndiyo mabingwa watetezi wa kombe la vilabu bingwa Ulaya wamefuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo baada ya kuichapa Arsenal kwa bao 3-1 kwenye mchezo wa marejeano uliochezwa kwenye uwanja wa Nou Camp.

Wakiwa wanaongoza kwa bao bao 2-0 za mchezo wa kwanza, Lionel Messi alishuhudiwa akimlazimisha David Ospina kufanya kazi ya ziada kuokoa shuti la karibu kutoka kwa nyota huyo kalba ya Neymar kupachika mpira kambani.

Mohamed Elneny aliisawazishia Arsenal bao hilo kipindi cha pili lakini Suarez aliongeza bao linguine na kuipa Barcelona uongozi wa bao 2-1.

Shuti la Danny Welbeck liligonga mwamba kabla Messi hajalizamisha kwa mara nyingine jahazi la Arsenal na kuwatupa nje ya mashindano kwa kukandamiza bao la tatu kwenye mchezo huo.

Ushindi huo unamaanisha Barcelona imefuzu kwenye hatua ya nane bora kwenye mashindano hayo kwa mara ya tisa mfululizo.

Lakini mbali na kufuzu hatua ya robo fainali ya Champions League, Barcelona imeendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo na kufikisha michezo 38 bila kupoteza kwenye michuano yote huku wakitafuta rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutetea ubingwa wa Ulaya.

Hakuna timu iliyofanikiwa kushinda Champions League mara mbili mfululizo tangu AC Milan ilipofanya hivyo mwaka 1989 na 1990.
Miamba hiyo ya Catalan bado ipo kwenye makombe yote msimu huu (Champions League, La Liga na Copa del Rey) huku wakiwa katika nafasi nzuri kwenye kila mashindandano.

Kikosi cha Luis Enrique kipo mbele kwa tofauti ya point nane kileleni mwa ligi ya Hispania zikiwa zimesalia mechi tisa na watacheza fainali ya Copa del Rey dhidi ya Seilla mwezi May.
QUARTER-FINALISTS
PSG
Benfica
Manchester City
Barcelona
Real Madrid
Wolfsburg
Atletico Madrid
Bayern Munich

STORI YA TATU;

Baada ya Juventus kuondoshwa kwenye michuano ya Champions League, mtandao wa ESPN umeandika kwamba, matokeo hayo ni habari njema kwa vilabu vya England Premier League.
Kipigo cha Juve kinamaanisha vilabu vya Premier League bado vitaendelea kupata nafasi nne kwenye michuano ya vilabu bingwa Ulaya katika msimu ujao 2017-18.
Kufanya vizuri kwa vilabu vya Italy kungepelekea kupoteza nafasi ya EPL kupeleka timu nne kwenye michuano ya Champions League lakini nafasi hiyo wameipoteza kutokana na Juve kuondolewa kwenye hatua ya 16 bora.

Juve kung’olewa na Bayern kuinaicha timu moja ya Serie A kwenye michuano ya Ulaya.
Lazio inaweza kuongeza ‘coefficient points’ hadi kufikia 2.5 endapo itafanikiwa kuchukua Europa League, lakini England hadi sasa tayari inapointi 3.97 mbele ya Italy.
Kama England itapeleka timu tatu pekee kwenye michuano ya Champions League basi ile dhana kwamba the Premier League ni bora duniani haita kuwepo tena.
England imeshindwa kufanya vizuri kwenye michuano ya Champions League kwa kushindwa kupeleka timu timu zaidi ya moja kwenye hatua ya robo fainali lakini pia hali ni tete katika Europa League ambapo Tottenham Hotspur ipo nyuma kwa magoli 3-0 dhidi ya Borussia Dortmund baada ya mchezo wa kwanza.
Timu kutoka Ujerumani na Hispania zimekuwa zikifanya vizuri zaidi ya zile za England msimu huu.
Vilabu vya Serie A vimepata pointi 19.00 msimu uliopita, mara ya kwanza vilivishinda vilabu vya Premier League tangu msimu wa 2005-06.
Vilabu vya italia vilitakiwa kufanya hivyo tena huku vilabu vya England vikiendelea kuboronga ili vinyang’anye nafasi nne ilizonazo England kwenye michuano ya Champions League.
Lakini nafasi ya Italy ilipotea baada ya Sampdoria kupigwa vibaya kwenye raundi ya tatu ya Europa League. Hiyo ikatoa mwanya kwa England ambayo vilabu vyake vya Southampton na West Ham pia vilishindwa kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyohiyo.
Kipigo cha Fiorentina dhidi ya Tottenham kwenye hatua ya 32 bora ya Europa League ilizidi kudidimiza ndoto zao, na kwa sasa hakuna nafasi ya Italy kuipiku England kuingiza vilabu vinne kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni