
Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga Aprili 24, mwaka huu, siku ambayo Azam FC itamenyana na Mwadui FC Uwanja wa Mwadui Complex, Tanga Aprili 24, mwaka huu pia.
Hiyo inafuatia droo iliyopangwa jana studio za Azam TV, wadhamini wa michuano hiyo, Tabata, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa.
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars, Esther Chabruma ndiye aliyechagua timu za kumenyana katika Nusu Fainali katika droo hiyo, akisimamiwa na Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto.
Coastal Union iliingia Nusu Fainali baada ya kuitoa Simba SC kwa kuifunga mabao 2-1, wakati Azam FC iliitoa Prisons kwa kuifunga 3-1, Mwadui FC iliitoa Geita Gold kwa kufunga 3-0 na Yanga SC iliwafunga Ndanda FC 2-1.
Bingwa wa Kombe la ASFC, michuano iliyoanza na timu 64 Novemba mwaka jana, ataiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.

Katika hatua ya awali, kila timu ilipatiwa fedha za usafiri Sh Milioni 3, na vifaa vya mashindano kutoka kwa wadhamini, Azam TV ikiwa ni sehemu ya udhamini wa Bilioni 3.3.
Bingwa wa Kombe la ASFC atajinyakuliwa kitita cha Sh. Milioni 50,
Fainali inatarajiwa kuchezwa wiki moja baada ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kumalizika.
Mara ya mwisho michuano hiyo ilifanyika mwaka 2002 na JKT Ruvu ikaifunga Baker Rangers ya Magomeni katika fainali, wakati ikijulikana kama Kombe la FAT (Chama cha Soka Tanzania).
ORODHA YA MABINGWA KOMBE LA SHIRIKISHO
1967 Yanga SC
1974 Yanga SC
1985 Maji Maji
1995 Simba SC
1996 Sigara
1997 Tanzania Stars
1998 Tanzania Stars
1999 Yanga SC
2000 Mtibwa Sugar
2001 Yanga SC
2002 JKT Ruvu
Chanzo: Bin Zubeir
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni