Manchester City wameshindwa kufika
katika fainali za kwanza za klabu bingwa barani Ulaya (UEFA) baada ya
kutolewa na mabingwa mara 10 wa michuano hiyo Real Madrid katika mchezo
uliokua wa kuvutia tena wa aina yake. Walichapwa 1-0.
Baada ya kutokuwa na ushindi wowote katika mzunguko wa kwanza, Real Madrid walianza kuongoza kipindi cha kwanza kufuatia mpira wa krosi uliopigwa na Gareth Bale kumbabatiza kiungo wa City Fernando na kuingia nyavuni.
Real waliutawala mchezo huku mpira wa kichwa uliopigwa na Bale ukigonga mwamba na baadaye mlinda mlango wa City Joe Hart akiondoa mikwaju ya Luka Modric na Cristiano Ronaldo.
Klabu hiyo ya Uingereza ilikuwa ikihitaji bao moja muhimu la ugenini hususan katika dakika za lala salama kuelekea fainali,lakini hilo halikuweza kufanikiwa licha ya kushangiliwa na mashabiki wake wapatao 4,500.
Madrid walipata wakati mgumu kidogo pale mkwaju mkali wa Sergio Aguero ulipogonga nyavu za juu za lango la Madrid.
Real sasa watakutana na Atletico katika uwanja wa San Siro tar 28 Mei, hii ikiwa ni kama marudio ya fainali za mwaka 2014 ambapo Real walishinda kwa mabao 4-1 baada ya muda wa nyongeza.
Real Madrid wameingia fainali ya 14 katika michuano ya vilabu bingwa barani Ulaya ,European Cup/Champions League,ikiwa ni rekodi na kufanikiwa kutwaa taji mara 10.
MATCH FACTS
Real Madrid (4-3-3):
Navas 7.5; Carvajal 7, Pepe 7.5, Ramos 8, Marcelo 7; Modric 8 (Kovacic
88 mins), Kroos 7, Isco 7.5 (Rodriguez 68, 6); Bale 8, Ronaldo 7.5, Jese
7.5 (Vasquez 56, 6)
Subs not used: Casilla, Varane, Danilo, Mayoral
Booked: Lucas
Goal: Fernando (og) 20
Manager: Zidane 7.5
Manchester City (4-2-3-1):
Hart 7; Sagna 6, Kompany (Mangala 10, 5.5), Otamendi 6.5, Clichy 6.5;
Fernando 6.5, Fernandinho 6.5; Navas 6 (Iheanacho 69, 6), Toure 5.5
(Sterling 61, 6), De Bruyne 6; Aguero 6
Subs not used: Caballero, Kolarov, Delph, Bony
Booked: De Bruyne, Fernando, Otamendi
Manager: Pellegrini 6
MOTM: Bale
Referee: Damir Skomina (Slovenia) 6
Attendance: 78,300
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni