BEKI
aliyetupiwa virago Simba SC ya Tanzania, Juuko Murshid amejumuishwa
katika kikosi cha mwisho cha Uganda cha wachezaji 19 kwa ajili ya mchezo
wa kirafiki dhidi ya Zimbabwe kesho.
Kikosi cha The Cranes kimeondoka asubuhi ya leo Kampala kwenda Harare kwa mchezo wa kirafiki na wenyeji, Zimbabwe kabla ya kumenyana na Botswana katika mchezo wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwishoni mwa wiki.
Katika kikosi hicho, Micho amemjumuisha pia mshambuliaji wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi ambaye kwa sasa anachezea SonderjyskE ya Denmark.
Kikosi kamili cha The Cranes kinaundwa; Denis Onyango, Robert Odongkara, Denis Iguma, Joseph Ochaya, Luwagga Kizito, Okwi Emma, Wasswa Hassan Mawanda, Juuko Murushid, Sekisambu Erisa, Kasirye Davis, Massa Geoffrey, Miya Faruku, Lorenzen Melvyn, Walusimbi Godfrey, Aucho Khalid, Lubega Idrisa, Isinde Isaac, Tony Mawejje na Yassar Mugerwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni