ZI |
Wakati
pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara likitarajiwa kufungwa
Jumapili Mei 22, 2016 kwa michezo minane, Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), limetoa onyo kali kwa timu zote kutojiingiza kwenye mtego wa aina
yoyote wa kupanga matokeo.
Rais
wa TFF, Jamal Malinzi ameziasa timu zote za Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, kucheza mechi hizo kwa kufuata taratibu, kanuni za Ligi
Kuu kadhalika sheria 17 zinazoongoza mchezo huo ambao unapendwa na
mamilioni ya watu Tanzania na dunia nzima.
“Nimefanya
tathmini yangu na kubaini kwamba, inawezekana kukawa na mipango ya
kupanga matokeo. Nichukue nafasi hii kuzionya timu zote kutojiingiza
hulo. TFF iko makini, tena makini sana na ina watu wake kila mkoa ambako
michezo hiyo itafanyika, sasa basi naziasa timu kufuata taratibu,
kanuni na sheria,” alisema Malinzi.
Mbali
ya Malinzi, pia Bod ya Ligi nayo imetoa onyo ikisema michezo yote haina
budi kuanza saa 10.00 jioni hata kama kutakuwa na hali ya mvua katika
viwanja husika lengo likiwa ni kukabiliana na upangaji wa matokeo.
Baada
ya michezo 29 kwa kila timu, tayari Coastal Union ya Tanga ikiwa imeaga
rasmi Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania 2015/16 na kwamba kuna timu tano
ambazo baadhi yake (timu mbili) zikipata matokeo mabaya zitaungana na
Wagosi wa Kaya kushuka daraja msimu wa 2015/16. Coastal Union yenye
pointi 22 na hata ikishinda mchezo wa mwisho, haiwezi kuzifikia timu
zilizo juu yake.
Timu
ambazo ziko kwenye hatari ya kushuka ni African Sports ya Tanga yenye
pointi 26 (nafasi ya 15); Mgambo pia ya Tanga iliyojikusanyia pointi 27
(nafasi ya 14); Kagera Sugar ya Kagera iliyovuna pointi 28 (nafasi ya
13); JKT Ruvu ya Pwani iliyopata pointi 29 (nafasi ya 12) na Toto
Africans ya Mwanza yenye pointi 30 (nafasi ya 11).
Kwa
hali ya mambo ilivyo, licha ya kwamba Toto inaweza kujihesabu ina nafuu
ikilinganishwa na timu nyingine, ukweli unabaki kuwa kwa timu zenye
pointi 27 hadi 29 zinaweza kuishusha kama Wanakishamapanda hao
watapoteza mchezo wa mwisho au kupata sare huku wapinzani wao
wakishinda.
Kwa
mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Toto Africans
itakuwa mwenyeji kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuikaribisha
Stand United, wakati JKT Ruvu mgeni wa Simba ya Dar es Salaam kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wenyewe
Kagera Sugar watamaliza na Mwadui FC watakuwa kwenye Uwanja wa
Kambarage Shinyanga wakati Mgambo wataalikwa Azam FC kwenye Uwanja wa
Azam Complex ulioko Chamazi-Mbagala, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam
ilihali African Sports ‘Wanakimanumanu’ wataifuata Mtibwa Sugar kwenye
Uwanja wa Manungu, Mvomero mkoani Morogoro.
Mechi
nyingine ya kukunja jamvi kwenye Ligi Kuu ya Vodacom zitakuwa kati ya
Mabingwa wa Ligi Kuu msimu huu, Yanga itakayokuwa mgeni wa Majimaji ya
Songea kwenye Uwanja wa Majimaji wakati Mbeya City itakuwa mwenyeji wa
Ndanda FC ya Mtwara.
Mchezo
mwingine wenye presha utakuwa ni kwa Tanzania Prisons yenye pointi 48
ambayo licha ya kucheza na Coastal Union ambayo imeshuka daraja kwenye
Uwanja wa Mkwakwani, itakuwa inafukuziwa na Mtibwa Sugar kuwa na nafasi
ya nne. Mtibwa Sugar ina pointi 47.
Tanzania
Prisons itacheza na timu ambayo haina nafasi katika Ligi Kuu msimu huu.
Presha kubwa ni kwa Simba na Azam ambazo zina tofauti ya pointi moja
katika msimamo wa ligi hiyo iliyoshirikisha timu 16.
Azam
FC ina pointi 63 ikishika nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Yanga huku
Simba inayoshika nafasi ya tatu ina pointi 62. Mvutano wa Tanzania
Prisons, Mtibwa ni wa nafasi ya tatu na nne hasa ukirejea kwenye zawadi
za Vodacom ka timu vinara kama ilivyo kwa Azam na Simba.
Yanga
ambayo imetwaa ubingwa, tayari imepewa taji na medali kwa wachezaji 24,
viongozi saba wa benchi la ufundi na viongozi wanne wa Kamati ya
Utendaji Jumamosi iliyopita na inachusubiri ni fedha Sh 81,345,723
wakati Azam na Simba zinawania zawadi ya mshindi wa Pili Sh 40,672,861
na Mshindi wa Tatu Sh 29,052,044 huku Prisons na Mtibwa Sugar zikichuana
kupata zawadi ya Mshindi wa Nne ambayo ni Sh 23,241,635.
Pia
timu zote zinawania zawadi ya Mchezaji Bora ambayo ni Sh 5,742,940
kiwango kinachofanana na atakachopewa Mfungaji Bora wa Ligi na Kipa Bora
wa michuano hiyo inayodhaminiwa na Vodacom wakati Mwamuzi Bora
atazawadiwa Sh 8,614,610 kiwango kinachofanana atakachopewa Kocha Bora
wakati timu yenye nidhamu itavuna Sh 17,228,820.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni