Wanachama
wa Yanga wakiongozwa na Baraza la Wazee la Yanga, wameliomba Jeshi la
Polisi Tanzania Kanda ya Ilala kuwaruhusu kufanya maandamano.
Wanachama
hao wamefikia uamuzi huo kwa madai kuna njama za magazeti ya Nipashe na
The Guardian yanayomilikiwa na Reginald Mengi kumchafua mwenyekiti wao,
Yusuf Manji.
Vita
hiyo, kati ya wanachama wa Yanga na magazeti hayo inazidi kuchukua kasi
baada ya wanachama wa Yanga kuyachoma na kuyachana ikiwa ni ishara ya
kuonyesha hasira zao.
Katibu wa Baraza la Wazee Yanga, Ibrahim Akilimali amewasilisha barua kwa Jeshi la Polisi kuomba maandamano hayo.
“Kweli nimefanya hivyo, tumechoka maana wanatusakama sana. Sisi tunataka maandamano ya amani kupinga hili.
“Manji
sasa si mkurugenzi wa makampuni yanayotajwa na magazeti hayo. Watuachie
afanye kazi za Yanga maana sasa ndiyo tumefuzu kucheza hatua ya robo
fainali.
“Wanamchanganya makusudi, tena wanafanya hivi kwa kuwa kipindi hiki Yanga imefuzu ndiyo wameanza kuandika stori zake.
“Mbona hawakuandika kabla Yanga haijafuzu, wanatuchanganya kwa makusudi,” alisema.
Bado haijajulikana kama Jeshi la Polisi litatoa ruhusa kwa wanachama hao kufanya maandamano katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Bado
wakuu wa magazeti hayo hawajatoa kauli yoyote kuhusiana na hatua hiyo
ya wanachama wa Yanga, hasa uamuzi wa kuyachana na kutyachoma moto.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni