Kwa hivi sasa Jose Mourinho anatamkwa kwenda kuchukua nafasi ya Muholanzi, Louis Van Gaal alietimuliwa kuifundisha Manchester United.
Uwepo wa Mourinho Old Trafford unasubiliwa kwa hamu kubwa sana kuona kama kocha huyo atarejesha mafanikio ya Mashetani wekundu katika kuchukua vikombe mbalimbali.
Ukiachilia mbali taarifa ya uwezekano wa Giggs kuikacha Manchester United kwa sababu za ujio wa Mourinho huku pia taarifa zikisema Mourinho anamuhitaji Gary Neville kwenye benchi la ufundi stori nyingine kubwa Pep Guardiola kocha mpya wa Manchester City.
Makocha hawa wamekuwa na ushindani mkubwa wa kimafanikio na pia walipokuwa wote Hispania. Mengi yanazungumzwa kuona ni nani kati yao atakuwa mbabe wa mwenzake.
Guardiola na Mourinho walipokuwa Barca 1990 chini ya kocha Sir Bobby Robson
MOURINHO ANAHAMA ZAKE LONDON, HUYOOOOO JIJINI MANCHESTER
Kocha Jose Mourinho ameonekana akisimamia kazi ya kuhama katika eneo la West London jijini London.
Wakati Mourinho anasimamia zoezi hilo, hakuna ubishi sasa anahamia jijini Manchester kwa ajili ya kuanza kazi mpya.
Baada
ya kocha Louis van Gaal kutupiwa virago licha ya kutwaa Kombe la FA,
kocha anayeelezwa anajiunga na Man United ni Jose Mourinho.
MOURINHO AKITAKA WACHEZAJI HAWA NA BEI ZAO...
Mara tu atakapotangazwa kuwa Kocha mpya wa Manchester United, kocha Jose Mourinho atataka kuboresha kikosi chake.
Wachezaji wengi sana anaweza kuwatazama lakini wake ambao bei zao ni juu na wengine wake huru kama Zlatan Ibrahimovich.
HAWA HAPA NA BEI ZAO, KAZI KWAKE
Nemanja Matic - Chelsea - £25million
Joao Mario - Sporting Lisbon - £35m
Antoine Griezmann - Atletico Madrid - £63m
Gonzalo Higuain - Napoli - £72m
John Stones - Everton - £45m
Raphael Varane - Real Madrid - £35m
Alvaro Morata - Juventus/Real Madrid - £40m
JEZI YA MAN UNITED NA JINA LA JOSE MOURINHO MTAANI
Tayari
jezi za Manchester United zenye jina la Kocha Jose Mourinho ziko
mtaani, hii inaonyesha namna gani watu wanajua kutumia fursa. Kocha huyo
anatarajia kujiunga rasmi na Manchester United ndani ya saa chache.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni