YANGA SC imepangwa kundi la A katika Kombe la Shirikisho Afrika pamoja na mabingwa wa zamani barani Afrika, TP Mazembe ya DRC, MO Bejaia ya Algeria na Medeama ya Ghana.
Kundi B linaundwa na timu za Kaskazini mwa Afrika tupu ambazo ni Etoile du Sahel ya Tunisia ambao ni mabingwa watetezi, Ahly Tripoli ya Libya, FUS Rabat na Kawkab zote za Morocco.
Ratiba hiyo inamaanisha Yanga itakutana na timu ya mshambuliaji wa Tanzania, Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya DRC.
Na mchezo huo ni kutimia kwa ndoto za Ulimwengu, ambaye wiki iliyopita alikakaririwa akisema ana hamu ya kupanga na Yanga.
Ulimwengu alisema anatamani katika droo ya CAF wapangwe na Yanga na atafurahi kucheza dhidi ya timu ya nyumbani. “Itakuwa mechi nzuri sana sisi na Yanga, yaani mimi nacheza pale Taifa dhidi ya Yanga, tamu sana,”alisema Uli maarufu kwa jina la Rambo mjini Lubumbashi.
Na mapema leo, kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Niyonzima anayechezea Yanga amesema kwamba sasa wana uzoefu wa kutosha wa mashindano makubwa baada ya kucheza mfululizo, hivyo hawaihofii timu yoyote watakayopangwa nayo.
“Katika kipindi cha miaka hii mitatu tumecheza na timu za Kaskazini mwa Afrika, Kusini na huku kwetu Mashariki, bahati mbaya hatujakutana na timu za Magharibi ambazo kwa sasa si tishio,”amesema Niyonzima.
Nahodha huyo wa Amavubi amesema kwamba katika kundi lolote watakaloangukia watapambana wafanye vizuri ili wafike mbali.
MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA;
Katika Ligi ya Mabingwa Afrika kundi A kuna timu za Zesco United ya Zambia, Al Ahly ya Misri, Asec Mimosa ya Ivory Coast, Waydad Casablanca ya Morocco, wakati Kundi B kuna Enyimba ya Nigeria, Zamalek ya Misri, ES Setif ya Algeria na Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini.
MAKUNDI KOMBE LA MABINGWA
RATIBA KOMBE LA SHIRIKISHO
KUNDI A:
Juni 17, 2016
MO Bejaia Vs Yanga SC
TP Mazembe Vs Medeama
Juni 28, 2016
Yanga SC vs TP Mazembe
Medeama Vs MO Bejaia
Julai 15, 2016
Yanga SC Vs Medeama
MO Bejaia Vs TP Mazembe
Julai 26, 2016
TP Mazembe Vs MO Bejaia
Medeama Vs Yanga SC
Agosti 12, 2016
Medeama Vs TP Mazembe
Yanga SC Vs MO Bejaia
Agosti 23, 2016
TP Mazembe Vs Yanga SC
Mo Bejaia Vs Medeama
KUNDI B:
Kawkab Marrakech Vs Etoile du Sahel
F.U.S Rabat Vs Ahly Tripoli
Juni 28, 2016
Etoile du Sahel Vs F.U.S Rabat
Ahly Tripoli Vs Kawkab Marrakech
Julai 15, 2016
Etoile du Sahel Vs Ahly Tripoli
Kawkab Marrakech Vs F.U.S Rabat
Julai 26, 2016
F.U.S Rabat Vs Kawkab Marrakech
Ahly Tripoli Vs Etoile du Sahel
Agosti 12, 2016
Ahly Tripoli Vs F.U.S Rabat
Etoile du Sahel Vs Kawkab Marrakech
Agosti 23, 2016
Kawkab Marrakech Vs Ahly Tripoli
F.U.S Rabat Vs Etoile du Sahel
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni