Michuano ya Copa America imefikia
tamati leo hii kwa mabingwa watetezi Chile kuendeleza ubabe wake dhidi
ya Vigogo wa soka duniani Argentina.
Mshambuliaji nyota wa Arsenal, Alexis Sanchez ametangazwa kuwa mwanasoka bora wa michuano ya Copa America.
amewapiku nyota wengine wengi wakiwemo Lionel Messi,
Angel Di Maria na wengine wengi.
Dakika 120 za mchezo huo zilishuhudia timu hizo zikienda suluhu ya bila kufungana.
Mchezo huo ulitawaliwa na ubabe wa hapa na pale huku ikushuhudiwa timu zote mbili zikimaliza kipindi cha kwanza zikiwa na wachezaji 10 baada ya Marcelo Diaz wa Chile kulambwa kadi mbili za njano na kuwa nyekundu dakika ya 28 kabla ya Marcos Rojo wa Argentina kutolewa nje dakika ya 43 kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja.
Katika upigaji wa penalti,Arturo Vidal wa Chile alianza kwa kukosa kabla ya Lionel Messi na Lucas Biglia kukosa kwa upande wa Argentina.
Hii inakuwa fainali ya pili ndani ya miaka miwili kwa timu hizi mbili kukutana katika hatua ya fainali amapo mara zote mbili Chile wamechukuwa kikombe hicho kwa mikwaju ya penalti.
Fainali hizi zilichezwa mwaka jana nchini Chile na kurudiwa mwaka huu ikiwa ni maadhimisho ya miaka 100 tokea kuanza kwa michuano hii mwaka 1916.
WAKATI HUO;
MESSI ASTAAFU KUICHEZEA ARGENTINA KWA KILIO NA MACHOZI
MAUMIVU
ya moyo yamemshinikiza Mwanasoka Bora wa Dunia, Lionel Messi kustaafu
kuichezea timu yake ya taifa ya Argentina baada ya jana kufungwa katika
fainali ya tatu mfululizo ya Copa America ndani ya miaka mitatu.
Messi
si mgonjwa wa moyo, bali ameumizwa n a kitendo cha kukosa penalti ya
kwanza Argentina ikifungwa kwa penalti 4-2 katika fainali ya Copa
America Centenario baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 120.
Lionel Messi amestaafu kuichezea timu yake ya taifa ya Argentina
Messi ambaye alimwaga machozi na kilio baada ya mechi hiyo alizungumza na Televisheni ya Argentina baada ya mechi na kufafanua uamuzi wake. "Ni hivyo. Mimi baso na timu ya taifa,"alisema.
Messi ambaye alimwaga machozi na kilio baada ya mechi hiyo alizungumza na Televisheni ya Argentina baada ya mechi na kufafanua uamuzi wake. "Ni hivyo. Mimi baso na timu ya taifa,"alisema.
"Si
kwangu. Hii ni fainali ya nne. Uamuzi umefanyika, nafikiri hivyo.
[kushinda] ndicho ninachoitaka zaidi. Sikuja. nafikiri ni hivyo. Hivyo
ndivyo ninavyojisikia kwa sasa, ninachofikiria. ni maumivu makubwa,".
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni