JARIDA maarufu la Forbes la Marekani limewataja wachezaji nyota Cristiano Ronaldo na Lionel Messi kuwa ndio wanamichezo wanaolipwa zaidi duniani.
Nyota wa Real
Madrid Ronaldo ndio anaongoza orodha hiyo kwa kukunja kitita cha paundi
milioni 60.9 katika kipindi cha miezi 12 iliyopita huku nyota wa
Barcelona Messi yeye akijikusanyia paundi milioni 56.3.
Nyota wa mchezo
wa gofu Tiger Woods na bondia Floyd Mayweather ndio waliokuwa wakitawala
orodha hizo kwa muongo mmoja uliopita lakini huku Woods akiandamwa na
majeruhi na kushuka kiwango na Mayweather akiwa amestaafu Ronaldo na
Messi wamepanda na kuongoza orodha hizo.
Ronaldo anakuwa mwanamichezo wa
pili kutoka katika timu baada ya nguli wa mpira wa kikapu Michael
Jordan kuongoza orodha hizo toka jarida hilo lilipoanza kukokotoa vipato
vya nyota vya wanamichezo mbalimbali mwaka 1990.
Nyota wengine waliopo
katika orodha hiyo ni nyota wa mpira wa kikapu Lebrone James anayeshika
nafasi ya tatu kwa kuingiza paundi milioni 53.4, nyota wa tenisi Roger
Federer yuko nafasi ya nne akiingiza paundi milioni 46.9 na nyota
mwingine wa mpira wa kikapu Kevin Durant anakamilisha tano bora kwa
kuingiza paundi milioni 38.6.
Neymar, Zlatan Ibrahimovic na Gareth Bale
ndio wachezaji soka wengine pekee waliopo katika orodha hiyo wakiwa
katika nafasi ya 21, 22 na 25 kwa kuingiza kiasi cha paundi milioni
25.8, 25.7 na 24.7.
2-VIDEO MPYA YA TANGAZO LA NIKE IKIMHUSISHA RONALDO.
3-HODGSON AWAFUNIKA MAKOCHA WOTE EURO 2016 KWA KULIPWA MKWANJA MREFU;
KOCHA wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson ndiye anayelipwa zaidi ya makocha wote wa Euro 2016, akiwa anaingiza kiasi cha Pauni Milioni 3.5 kwa mwaka akimpiku Antonio Conte wa Italia, anayefuatia kwa kulipwa Pauni Milioni 3.15 na Fatih Terim wa Uturuki anashika nafasi ya tatu kwa kulipwa Pauni Milioni 2.7.
Makocha wanane kati ya 24 wanaingiza Pauni Milioni kila mmoja kwa mwaka - lakini mmoja tu, Leonid Slutsky haingizi kitu.
Slutsky pia ni kocha wa CSKA Moscow na amechukua majukumu ya timu yake ya taifa kuokoa jahazi baada ya Fabio Capello kuondoka.
Wakati Slutsky anapewa timu ya taifa majira ya joto yaliyopita, Waziri wa MIchezo Vitaly Mutko alithibitisha: "Hatakuwa na mshahara, isipokuwa posho kulingana na matokeo,".
4-RONALDO AIPA NAFASI ITALIA KUTWAA EURO 2016.
MSHAMBULIAJI nyota wa
kimataifa wa Ureno, Cristiano Ronaldo ameitaja Italia kama moja ya timu
ambazo zinaweza kutwaa taji la michuano ya Euro 2016.
Hatua hiyo inaweza kuwa ya kushangaza haswa kutokana na mara kadhaa Italia kutopewa nafasi kutokana na kukosa nyota wenye ubora katika kikosi chao.
Italia inaingia katika michuano hiyo ikiwa bila ya viungo wake mahiri Marco Verratti na Claudio Marchisio ambao wameachwa kutokana na kuwa majeruhi.
Hata hivyo, Ronaldo anaamini Italia ambao hawajafungwa katika mechi zao za kufuzu michuano hiyo, ni moja timu zenye nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo sambamba na Ufaransa, Ujerumani na Italia.
Ureno imepangwa katika kundi F katika michuano hiyo sambamba na Iceland, Austria na Hungary.

5- MAJERUHI YAMLAZIMISHA AGGER KUTUNDIKA DARUGA MAPEMA.
BEKI wa zamani wa
Liberpool, Daniel Agger amestaafu rasmi soka lake akiw ana umri wa miaka
31.
Agger ambaye amekuwa akisumbuliwa kwa kipindi kirefu cha soka lake la majeruhi aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kuelezea uamuzi wake huo.
Agger aliandika katika twitter akiwashukuru wale wote waliomuunga mkono katika kipindi chote na kuongeza japo ni uamuzi mgumu lakini anadhani ni sahihi kwa afya yake.
Beki huyo wa kimataifa wa Denmark ambaye aliondoka Liverpool mwaka 2014 baada ya kuitumikia kwa miaka nane na kurejea katika klabu yake ya utotoni ya Brondby, amewahi kuichezea nchi hiyo mechi 75.

6- POGBA ATAMANI KUWA KAMA KINA PELE NA MARADONA.
KIUNGO wa zamani wa
Manchester United, Paul Pogba amesisitiza kuwa anataka kukumbukwa kama
ilivyo kwa nguli wengine kama Diego Maradona wa Argentina na Pele wa
Brazil.
Kiungo wa anayekipiga Juventus, amesema amepania kufikia malengo yake hayo kwa kujituma na kuhakikisha kila siku anaimarika.
Pogba ameimarika na kuja kuwa mmoja kati ya wachezaji bora kabisa kwasasa toka aondoka United kuelekea Turin mwaka 2012 ambapo ameisaidia Juventus kunyakuwa mataji manne mfululizo ya Serie A na kufika fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2015.
Akihojiwa na luninga ya ESPN, Pogba amesema kwasasa hadhani kama ameshafanya lolote katika soka kwani bado kuna mataji mengi hajawahi kushinda kama Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la Dunia na hata Euro.
Pogba mwenye umri wa miaka 23 aliendelea kudai kuwa malengo yake ni kuendelea kuimarika na kuhakikisha anashinda kila kitu.

7- ADIDAS WAOMBA RADHI KWA KUKOSEA JINA LA COLOMBIA.
KAMPUNI
ya vifaa vya michezo ya Adidas imeomba radhi kwa kuandika vibaya jina
la Colombia katika matangazo yake yanayohusu jezi mpya wanazotumia timu
ya taifa ya nchi hiyo katika michuano ya Copa America.
Tangazo hilo ambalo linawaonyesha wachezaji wa Colombia wakiwa katika jezi nyeupe liliondolewa baada ya mitandao ya kijamii kushambulia kwa kwa kuliandika vibaya jina la nchi hiyo ambap waliandika Columbia badala ya Colombia.
Katika taarifa yake kampuni hiyo yenye makao yake makuu huko Portland, Oregon imedai kuwa wanathamini ushirikiano wao na Shirikisho la Soka la Colombia na kuwaomba radhi kwa makosa hayo yaliyofanyika.
Adidas wamekuwa wakitengeneza sare za Colombia toka mwaka 2011.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni