Ligi ya mabingwa barani Afrika pamoja na shirikisho kwenye hatua ya makundi inaanza rasmi siku ya leo jumamosi.
Mashindano hayo makubwa zaidi kwa ngazi ya vilabu Afrika yamekuwa na ushindani wa hapa na pale kutokana na vipaji vikubwa vya soka katika bara hili.
Kombe la mabingwa linahusisha vilabu nane ambavyo vimegawanywa katika makundi mawili kundi A ni Zesco United (Zambia), Al Alhly(Misri),ASEC Mimosas (Cote Dvoire),Wydad
Casablanca (Morocco) na kundi B ni,ES Setif (Algeria),Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini),Enyimba (Nigeria) pamoja na Zamalek ya Misri.
Upande wa kombe la shirikisho barani Afrika vilabu shindani ni nane ambavyo navyo vimegawanywa katika makundi mawili A na B, katika kundi A ni TP Mazembe (DRC), Medeama (Ghana) ,MO Bejaia (Algeria) ,Yanga FC (Tanzania) na kundi B ni FUS Rabat(Morroco) , Kawkab Marrakech (Morroco) ,Al Ahli Tripoli (Libya) na Étoile du Sahel ya Tunisia.
Jumamosi Juni 18 2016
Zesco United (Zambia) vs Al Alhly(Misri)-Saa 10:30 Jioni.
ASEC Mimosas (Cote Dvoire) vs Wydad
Casablanca (Morocco) saa 13:30 Mchana.
ES Setif (Algeria) vs Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)-Saa 6:15 Usiku.
Jumapili Juni 19 2016
Enyimba (Nigeria) vs Zamalek(Misri) -Saa 12:00 Jioni.
RATIBA YA KOMBE LA SHIRIKISHO.
Jumapili Juni 19 2016
TP Mazembe (DRC) vs Medeama (Ghana) –Saa 10:30 Jioni.
MO Bejaia (Algeria) vs Yanga FC (Tanzania)- Saa 6:15 Usiku.
Jumatatu Juni 20 2016
FUS Rabat(Morroco) vs Al Ahli Tripoli (Libya)- Saa 7:00 Usiku.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni