Kocha msaidizi wa klabu ya Yanga Juma Mwambusi amevunja ukimya na
kutoka ufafanuzi kuhusu watu wanaobeza kiwango cha mshambuliaji wa
kimataifa wa Zambia Obrey Chirwa aliyesajiliwa na klabu hiyo hivi
karibuni.
Wadau wengi wa soka nchini ikiwa ni pamoja na baadhi ya mashabiki wa
Yanga wamekuwa wakihoji uwezo wa nyota huyo aliyesajiliwa akitokea klabu
ya FC Platinum ya Zimbabwe.
“Ni moja ya wachezaji wazuri wa Yanga ambao wameongezwa lakini kwa
muda aliocheza bado hajazoea mfumo kwasababu kila klabu imacheza kwa
mfumo wake kwahiyo anatakiwa endane na mfumo wetu kwanza.
Chirwa ni
mgeni Yanga, anatakiwa kuzoea mazingira na mfumo wa mwalimu na anazoea
taratimu tuwe na subira,” alifafanua Mwambusi wakati alipofanyiwa
mahojiano na chombo kimoja cha habari.
“Tumemuona anamuelekeao, tumpe muda atakuwa kwenye kiwango kizuri
baada ya muda. Alivyokuja Ngoma mwazoni watu waliona kama hawezi lakini
alikuja kufanya kazi nzuri baadae.”
“Yanga imeingia kwenye makundi kwa mara ya kwanza baada ya muda
mrefu. Lakini watu wanataka matokeo, hapohapo tupate kombe na kila kitu,
ikitokea ndiyo lengo letu kubwa sisi waalimu na wachezaji kupata
matokeo mazuri lakini kama ikishindikana basi inatusaidia kupata
uzoefu.”
Hadi sasa Chirwa amecheza mechi tatu akiwa na Yanga, mechi ya kwanza
ilikuwa dhidi ya TP Mazembe kwenye uwanja wa taifa, akacheza tena dhidi
ya Medeama Yanga ilipokuwa kwenye uwanja wa taifa kabla ya kucheza tena
dhidi ya Medeama katika mchezo wa marejeano jana nchini Ghana.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Jumanne, 26 Julai 2016
BAADA YA KICHAPO MWAMBUSI AFUNGUKA KIWANGO CHA CHIRWA.......
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni