AZAM FC iko mbioni kukamilisha usajili wa mshambuliaji Yannick Zakri wa ASEC Mimosa ya Ivory Coast.
Mkurugenzi mmoja wa Azam FC anatarajiwa kuondoka Dar es Salaam kwenda Abidjan, Ivory Coast kumalizana na Zakri na ASEC.
Na mpango huo unakuja wakati tayari, Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Saad Kawemba yupo Ghana kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Enoch Atta Agyei.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Windy Professionals aliivutia Azam FC akiichezea Medeama wiki tatu zilizopita Dar es Salaam katika mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho.
Yannick Zakri (kulia) katika moja ya mechi za ASEC mjini Abidjan
Kinda huyo wa miaka 17, alifunga mabao 17 katika Ligi Daraja la Kwanza ya GN Bank akiwa na Windy Professionals kabla ya kuhamia Medeama SC mwaka jana.
Wachezaji wote hao wanatarajiwa kuwa wamekamilisha usajili wao na kujiunga na Azam FC hadi mwezi ujao – itategemea na klabu zao kama zitafika mbali kwenye michuano ya Afrika.
Yannick Zakri anaweza kutua Azam |
Aidha, katika wachezaji wote waliojitokeza kwa majaribio Azam FC, kocha Mspaniola Zeben Hernandez Rodriguez ameagiza wawili tu wasajiliwe ambao ni kipa Muivory Coast, Daniel Techi Yeboah na beki Mzimbabwe Bruce Kangwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni