Kaseja anaungana na kikosi hicho kuelekea Madagascar kwa ajili ya kambi ya wiki moja kabla ya kuikabili Afrika Kusini.
Kaseja ameiambia Goal, anashukuru kuona Shirikisho la soka Tanzania TFF, likimwamini na kumpa kazi hiyo na kuahidi kuwafua vizuri makipa hao wa timu ya vijana.
“Nimefurahi kwa TFF, na benchi la ufundi la Serengeti chini ya kocha Bakari Shime kwa nafasi hii nitajitahidi kutumia uzoefu wangu kuwanoa vijana hawa ili timu yetu iweze kufuzu fainali za vijana,”amesema Kaseja.
Kaseja anaungana na kikosi hicho kuelekea Madagascar kwa ajili ya kambi ya wiki moja kabla ya kuikabili Afrika Kusini kwenye mchezo wa kuwania kufuzu fainali hizo za mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa miaka 17.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni