STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 27 Julai 2016

WAMEVUTA MKWANJA MREFU PASIPO KUONESHA UBORA WAO VPL.........

 

Ligi Kuu Bara imezidi kubamba misimu ya miaka mitatu ya mwisho, lakini kuna wachezaji kutoka nje waliopiga fedha za bure pasipo kuonesha kiwango .

 

Msimu mpya 2016/2017 unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi wa nane, timu zipo katika kipindi cha usajili kwa ajili ya kuimarisha timu zao kwenye maeneo yenye mapungufu, wachezaji kutoka nje ya Tanzania wapo kwenye klabu tofauti-tofauti hasa Azam FC na Simba SC kwa ajili ya majaribio.

Lakini swali la msingi, Je! watasajili wachezaji wenye tija kwa klabu na Ligi Kuu au mwendo utakuwa ni ule wa kusajili wapiga pesa ilihali wana viwango dhaifu?

Msimu uliopita Ligi Kuu Bara tulishuhudia wachezaji waliosajiliwa kwa mbwembwe nyingi huku wakipewa madau makubwa lakini wakashindwa kuthibitisha umahiri wao dimbani. Haitapendeza kama msimu huu mambo yatajirudia kwa namna ile. Ipo orodha hapa ya wachezaji wa hovyo ambao wamefanya Ligi Kuu shamba la bibi kwa kusajiliwa kwa fedha nyingi lakini hawakuwa zalishi kwa klabu zao.

Alan Wanga | Azam FC
Alijiunga na Azam kwa pesa nyingi akitokea El Marrekh ya Sudan na alitarajiwa kufanya makubwa chini ya Stewart Hall lakini alishindwa, na muda mwingi akiambulia kusugua benchi mbele ya John Bocco na Kipre Tchetche ambao walionekana kuwa na mchango na athari kubwa dimbani, na hata alipopata nafasi hakuweza kuitumia vizuri na kwa msimu mzima akimaliza na goli moja tu Ligi Kuu Bara.

Paul Kiongera | Simba
Tayari amejiunga na AFC Leopard ya nchini kwao Kenya akitokea Simba, Muda mwingi alikuwa akitibu majeraha kuliko kucheza, alikuwa akilipwa mshahara mkubwa kuliko wazawa ambao walikuwa na faida kwenye klabu kuliko Mkenya huyo.

Issafou Boubacar | Yanga SC
Alisajiliwa kuja kuziba pengo la mbrazili Coutihno, ila hakufanya vizuri kama matarajio ya wengi alifanikiwa kucheza vizuri kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi kule Zanzibar, amevuna pesa nyingi ndani ya klabu bila mchango wowote.

Racine Diouf | Azam FC
Hakuwa na faida ndani ya Azam FC na hakufanikiwa kucheza mbele ya wazawa Morris, Mwantika, na Erasto Nyoni na tayari Azam imevunja mkataba naye na ameamua kurudi kwao Ivory Coast.

Brian Majwega | Simba
Ameshindwa kulizoea soka la Tanzania baada ya msimu mzima kumaliza na goli moja, usajili wake ulikuwa mkubwa nchini hasa baada ya Simba kumchukua akitokea Azam FC, kama Ilivyo kwa Kiongera, naye ameamua kurudi nyumbani kwao nchini Uganda.

Abasalim Chidiebele | Coastal Union
Msimu wa 2014/2015 alifanya vizuri sana akiwa na Stand United na kuivutia Coastal Union kumsajili kwa pesa nyingi, tofauti na matarajio Mnigeria huyu msimu wa 2015/2016 hakuweza kufanya lolote ndani ya Coastal Union  na kupelekea timu kushuka daraja.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox