KOCHA
Mkuu timu ya Mpira Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa
ameita kikosi cha wachezaji 24 watakaoanza kambi ya awali kuajindaa na
mchezo dhidi ya Nigeria utakaofanyika Lagos, Septemba 2, 2016.
Kwa
mujibu wa Mkwasa, timu hiyo itaingia kambini Agosti 1, 2016 na itadumu
kwa siku tano tu kabla ya kuvunjwa na kuitwa tena mwishoni mwa mwezi
Agosti, 2016 kujiandaa na kambi ya mwisho na moja kwa moja itakuwa ni
kwa ajili ya safari kwenda Nigeria.
Katika
kikosi hicho, Mkwasa hajawaita Nahodha, Mbwana Samatta wa KRC Genk ya
Ubelgiji na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo (DRC) kwa sababu ya majukumu waliyonayo kwenye klabu zao kwa
sasa.
Kadhalika,
nyota hao wataungana na wenzao nchini Nigeria kwa kuwa mchezo huo upo
kwenye kalenda ya CAF na ni wa mashindano. Mchezo huO ambao ni wa
kukamilisha ratiba, Mkwasa amesema utakuwa mgumu kwani Nigeria
wamebadili benchi la ufundi hivyo kila timu inaungalia mchezo huu kwa
jicho la pekee.
Wachezaji
walioitwa ni Makipa; Deogratius Munishi (Yanga), Aishi Manula (Azam) na
Benny Kakolanya (Prisons), mabeki; Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey
Morris (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Mohamed Husein ‘Tshabalala’
(Simba), Juma Abdul (Yanga) na Erasto Nyoni (Azam).
Viungo:
Himid Mao, Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya, Jonas Mkude, Ibrahim Jeba,
Mwinyi Kazimoto, Farid Mussa, Juma Mahadhi na Hassan Kabunda, wakati
washambuliaji ni Simon Msuva, Joseph Mahundi, Jamal Mnyate, Ibrahim
Ajib, John Bocco na Jeremia Juma.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Jumanne, 26 Julai 2016
MKWASA AMETANGAZA KIKOSI CHA WACHEZAJI 24 WA TAIFA STARS, KUIWINDA NIGERIA
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni