KLABU
ya Manchester United imekamilisha uhamisho wa kiungo wa kimataifa wa
Ufaransa, Paul Labile Pogba kwa dau la rekodi ya dunia, Pauni Milioni
100 kutoka Juventus ya Italia.
Kiungo huyo aliyekuwa anatakiwa na timu nyingi kubwa duniani, ikiwemo Real Madrid, aliwasili kutoka Juventus jana na kujiiunga na klabu yakzamani, ambayo aliiacha mwaka 2012.
Pogba mwenye umri wa miaka 23 anatarajiwa kuvaa jezi namba 6 na amesaini Mkataba mnono wa miaka mitano kwa mshahara wa Pauni 290,000 kwa wiki kufanya kazi chini ya kocha Mreno, Jose Mourinho.
Kuna kipengele pia cha kuongezwa mwaka mmoja katika Mkataba huo.
Paul Pogba akiwa na jezi ya Manchester United kwa mara ya kwanza baada ya kukamilisha usajili wake usiku wa kuamkia leo
Akizungumza
na tovuti ya klabu hiyo baada ya kusaini, Pogba alisema:
"Nina furaha
kujiunga tena na United. Imekuwa klabu yenye nafasi maalum katika moyo
wangu wakati wote na ninaangalia mbele kuelekea kufanya kazi na
Jose Mourinho.
"Nimefurahia
maisha yangu nikiwa na Juventus na nina kumbukumbu fulani nzuri za
klabu kubwa na wachezaji ambao ninaweza kuhesabu kama marafiki. Lakini
nafikiri ni wakati mwafaka kurejea Old Trafford.
Pogba akishuka katika gari na mama yakeYeo Moriba\
"Wakati
wote nafurahi kucheza mbele ya mashabiki na siwezi kusubiri kutoa
mchango wangu kwenye timu. Hii ni klabu sahihi kwangu kushinda kitu
chochote nachotumai kwenye mchezo,".
Kocha
Jose Mourinho alimsifu Pogba na akasema anaamini atadhuhirisha thamani
yake katuika urejeo wake kwenye klabu, akisema: "Paul ni mmoja kati ya
wachezaji bora duniani na atakuwa mtu muhimu katika timu ya United
nayotaka kujienga hapa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni