KLABU ya West Ham United imekamilisha rasmi usajili wa mshambuliaji Andre Ayew kutoka Swansea City kwa kitita cha paundi milioni 20.5.
Ayew mwenye umri wa miaka 26 alisajiliwa Swansea akiwa mchezaji huru akitokea Marseille Juni mwaka 2015 na kufanikiwa kufunga mabao 12 katika msimu wake wa kwanza Ligi Kuu.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ghana ambaye alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa BBc mwaka 2011, amesaini mkataba wa miaka minne na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyesajiliwa ghali na klabu hiyo.
Akihojiwa mara baada ya kukamilisha usajili wake, Ayew amesema klabu hiyo ina malengo mazuri ya kusonga mbele na anashukuru kuwa sasa nay eye atakuwa sehemu ya malengo hayo.
Ayew anakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa na West Ham kiangazi hiki wakati wakijiandaa kuanza msimu mpya katika Uwanja wa London.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni