STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 10 Agosti 2016

HUKU TUKIISUBIRI KWA HAMU MSIMU MPYA VPL, RATIBA YAPANGULIWA KIDOOGO

BODI ya Ligi (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imelazimika kubadili Ratiba ya Ligi Kuu kwa michezo kadhaa ya mwanzo kama kutokana sababu zilizo nje ya uwezo wao kama ifuatavyo.

1. Mchezo Na. 2 - Kagera Sugar vs Mbeya City (20.08.2016)
Mchezo huo sasa utachezwa tarehe 21.08.2016 katika Uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga. Sababu ni kuwa uwanja wa Kaitaba bado utakuwa kwenye matengenezo.

2. Mchezo Na.4 - Toto African vs Mwadui FC (20.08.2016)
Mchezo huo sasa utachezwa tarehe 24.08.2016 katika Uwanja wa CCM Kirumba. Sababu za mabadiliko ni kuwa uwanja huo tarehe 20.08.2016 utakuwa na matumizi mengine ya kijamii.

3. Mchezo Na.13 - Kagera Sugar vs Stand United (27.08.2016)
Mchezo huo sasa utachezwa katika Uwanja wa CCM Kambarage. Awali timu mwenyeji wa mchezo huo ilikuwa ni Kagera Sugar, lakini kwa sasa timu mwenyeji atakuwa ni Stand United.

4. Mchezo Na.55 - Toto vs Ndanda (02.10.2016)
Mchezo huo sasa utachezwa tarehe 03.10.2016 badala ya tarehe 02.10.2016

5. Mchezo Na.80 - Mbao FC vs Ndanda fc (16.10.2016)
Mchezo huo umerudishwa nyuma kutoka tarehe 16.10.2016 hadi tarehe 28.09.2016. Sababu ni kuiwezesha timu ya Ndanda kucheza michezo miwili kwa kanda ya ziwa kwa lengo la kupunguza gharama.

6. Mchezo Na.96 - Tanzania Prisons vs Mbao FC (22.10.2016)
Mchezo huo sasa utachezwa tarehe 23.10.2016 badala ya 22.10.2016 ili kuipa nafasi timu ya Mbao kupumzika na kusafiri. Tayari timu za Ligi Kuu ya Vodacom zimearifiwa na kuagizwa kuzingatia mabadiliko hayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox