Katika orodha hio mpya Tanzania imeshka kwa nafasi moja na kutoka nafasi ya 123 hadi nafasi ya 124 katika mwezi ambao haikucheza mechi yoyote inayozihusisha timu za wakubwa.
Kwa upande wa ukanda wa Afrika Mashariki, Uganda wanaendelea kuongoza baada ya kupanda na kufikia nafasi ya 65 duniani
Kwa ngazi ya bara, viwango hivyo vimeonyesha kuwa kwa Afrika, Algeria inaongoza ikifuatiwa na Ghana, Ivory Coast na Senegal ikishika nafasi ya nne.
Argentina bado kinara katika orodha hio ambao haina mabadiliko yoyote katika nafasi 19 za juu zaidi.
Nafasi ya pili inashikwa na Ubelgiji, nafasi ya tatu Colombia, nafasi ya nne Ujerumani na nafasi ya tano ikishikiliwa na Chile.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni