MSHAMBULIAJI mkongwe, Mussa Hassan Mgosi amestaafu rasmi soka na sasa anakuwa Meneja wa timu ya Simba SC.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Hajji Sunday Manara amesema kwamba Mgosi ataagwa rasmi katika mchezo wa kirafiki dhidi ya URA ya Uganda Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Na Manara amesema kwamba aliyekuwa Meneja wa timu, Abbas Suleiman Ally anakuwa Mratibu wa timu kuanzia leo na Nahodha mpya ni Jonas Gerald Mkude.
Aidha, Manara amesema kiungo Peter Mwalyanzi aliyesajiliwa msimu uliopita kutoka Mbeya City, ametolewa kwa mkopo African Lyon iliyopanda Ligi Kuu msimu huu.
“Kulingana na usajili uliofanyika msimu huu, timu sasa itakuwa na viungo wengi na ushindani wa namba utakuwa mkubwa, hivyo tumeona Mwalyanzi tumpeleke African Lyon kwa mkopo akapate nafasi ya kutunza kipaji chake,”.
“Kama atafanikiwa kukuza kiwango na mwalimu akajiridhisha, basi atarejeshwa huko mbele ya safari,”alisema.
Kikosi cha Simba SC kinaingia kambini leo Ndege Beach Hotel, Mbweni kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya URA Jumapili Uwanja wa Tafa.
Na mashabiki wa Simba SC watapata fursa ya kukishuhudia kikosi chao kwa mara ya pili wiki hii, kitakapomenyana na URA.
URA wanatarajiwa kuwasili leo na kesho watacheza mechi ya kwanza ya kujipima nguvu dhidi ya Azam FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Alhamisi, 11 Agosti 2016
MUSSA HASSAN MGOSI ATUNDIKA DARUGA RASMI, APEWA SHAVU MSIMBAZI
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni