Taarifa ya Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Hajji Sunday Manara imesema kwamba kikao hicho kilichofanyika hoteli ya Serena, Dar es Salaam kilikuwa muendelezo wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa klabu Julai 31.
Manara alisema katika kikao cha juzi, Dewji aliwaeleza rasmi Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba dhamira yake ya kununua asilimia 51 ya hisa za klabu kwa Sh. Bilioni 20.
Anataka kuitoa klabu kwenye Bajeti ya Bilioni 1.2 kwa mwaka hadi Bilioni 5.5 na kwa kuamini mashabiki wa Simba wanahitaji mafanikio ya haraka, ameahidi kusajili vizuri, tuajiri kocha mzuri, ambavyo vyote vinaweza kugharimu Sh. Bilioni 4 na kwamna Bilioni 1.5 itakayobaki, ataiweka katika mradi wa ujenzi wa Uwanja.
Mo Dewji ni mpenzi na mwanachama wa Simba SC, ambaye kati ya 1999 na 2005 alikuwa mdhamini Mkuu wa klabu na akazishawishi pia Simba Cement na NBC kuwekeza katika klabu hiyo hadi ikafuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2003 ikiitoa Zamalek ya Misri.
Mo pia amewahi kuwa mdhamini wa Singida United na mmiliki wa African Lyon kwa muda, kabla ya kuiuza kwa mfanyabishara Rahim ‘Zamunda’ Kangenzi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni