MENEJA wa Manchester United, Jose Mourinho anategemea mabingwa wa Ligi Kuu Leicester City kuanza wakiwa imara kutetea taji lao baada ya kuonyesha kiwango kizuri wakati wa maandalizi ya msimu mpya.
Mourinho pia amevutiwa na usajili uliofanywa na klabu hiyo baada ya kuwanasa nyota kama Ahmed Musa na Bartosz Kaputska na anamini Leicester wameimarisha kikosi chao kuliko kile kilichoishangaza dunia kwa kutwaa taji msimu uliopita.
Lakini Mourinho anafahamu ugumu wa kutetea taji na anaamini michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inaweza kuwarudisha nyuma kidogo Leicester walio chini Claudio Ranieri.
Mourinho amesema msimu ujao utakuwa tofauti kwao lakini anadhani wanaweza kubadilika kutokana na mazingira kwani ndio mara yao ya kwanza kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
United ambao walikuwa mabingwa wa Kombe la FA msimu uliopita wanatarajiwa kupambana na Leicester katika mchezo wa ngao ya hisani unaotarajiwa kufanyika kesho katika Uwanja wa Wembley.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni