Simba SC imeeanza vyema harakati ya kusaka ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya leo kuibuka na ushindi wa goli 3-1 mbele ya Ndanda FC katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijin Dar es salaam.
Katika mchezo huo ambao Simba SC walitawala mchezo wote na huku wakitengeneza nafasi kadhaa za kufunga na kutmia chache kati ya hizo.
Alikuwa Laudit Mavugo aliyefunguwa ukurasa wa mabao hii leo kwa kuifungia Simba SC goli la kwanza katika dakika ya 19.
Kuingia kwa goli hilo kuliwafanya Ndanda FC kucheza kwa tahadhari na huku wakipeleka mashambulizi ya kushtukiza na katika dakika ya 37 Ndanda FC walisawazisha goli hilo kupitia kwa Omari Mponda aliunga mpira wa adhabu wa Kiggi Makasi na kupeleka mchezo kwenda mapumziko wakiwa mbele sare ya goli 1-1.
Kuningia kwa goli hilo kuliwapa utawala wa mchezo Ndanda FC na kutengeneza nafasi mbili za kuongeza magoli ambazo walishindwa kuzitumia.
Kipindi cha pili Simba SC walikianza kwa kasi na kutawala mchezo kwa kipindi chote hicho na kuwafanya Ndanda SC kuzuia kwa wakati mwingi.
Katika dakika ya 73 mshambuliaji aliyetokea benchi Fredrick Blagnon kuchukuwa nafasi ya Ibrahim Ajibu alinunga kwa kichwa kona na Mohammed Hussein na kuiandikai Simba SC goli la pili.
Wakati Ndanda FC wakijiuliza walijikuta wanaruhusu goli la tatu kupitia kwa Ramadhan Kichuya katika dakika ya 79 akimalizia mpira uliotemwa na kipa wa Ndanda Chove akizuia mpira wa kona, na kupeleka mchezo kumalizika kwa Simba Sc kuibuka na ushindi wa goli 3-1.
Katika uwanja wa CCM Kambarage Standi united wametoka sare ya bila kufungana na Mbao FC katika ufunguzi wa ligi kuu ya vodacom hii leo.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Jumamosi, 20 Agosti 2016
MNYAMA AUNGURUMA TAIFA, MAVUGO AONGOZA MAUAJI
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni