STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 19 Agosti 2016

TIZAMA VIDEO GOLIKIPA AKITAFUTA HIRIZI ALIYOPOTEZA HUKO KILOSA................

 


Ligi daraja la nne inayowakutanisha mabingwa wa Wilaya katika kituo cha Kilosa  uwanja wa Azimio mkoani Morogoro ilimalizika kwa staili ya aina yake mara baada ya kutokea kituko kwenye mchezo huo.
 



































Mtendeni fc ya Kilosa ilipambana na  Vijana fc ya Gairo hadi dakika 90 za mwamuzi Kasimu Salehe zinakwisha Mtendeni fc ilitoka kifua mbele kwa kuibamiza Vijana Gairo kwa magori 4 kwa 1.

Magori ya Mtendeni fc yalifungwa na Shabani Makubi,Nasibu Kasimu aliefunga mawili na Juma Sefu Momo na gori la kufutia machozi la Vijana Gairo limefungwa na Baraka Msanya.


 Ulikuwa ni mchezo mgumu sana na mapumziko Mtendeni fc ya Kilosa na Vijana fc ya Gairo walikuwa wamefungana goli  1 kwa 1.

Baada ya mwamuzi kupiga firimbi ya mapumziko alionekana golini kipa wa Vijana Gairo kuna kitu anatafuta golini kwake ndipo wachezaji wote wa Vijana Gairo wakaungana na golikipa wao kutafuta hicho kitu baada ya uchunguzi ikaonekana golikipa ameangusha Hirizi na wenzie wakawa wanamlaumu kwa uzembe.

Cha ajabu wachezaji wa Vijana fc hawakwenda kupata mawaidha ya mwalimu wao mpaka mwamuzi anapiga firimbi ya kuanza kipindi cha pili wao Vijana fc wanaendelea kutafuta Hirizi hali iliyoleta vichekesho na mzaha toka kwa mashabiki.

Baada ya mchezo kumalizika mshambuliaji wa Mtendeni fc ''Nasibu Kasimu'' aliyepachika goli 2 alienda kwa Vijana fc na kumkabidhi golikipa Hirizi yake.

Tulipo muhoji Nasibu aliipataje hiyo Hirizi alisema aliiyona pindi inamdondoka golikipa huyo ndipo alipoiokota na kuiweka  katika soksi yake na kufanikiwa kufunga goli 2  na hadi mwisho wa mchezo Mtendeni fc 4 na Vijana fc gairo 1.

kwa mujibu wa msimazi wa kituo cha Kilosa Bonifasi Kiwale akathibisha kuwa Mtendeni fc ndio mabingwa wa kituo cha Kilosa baada ya kufikisha point 7 na timu ya Halimashauri ya Gairo ni washindi wa 2 wa kituo baada ya kuwa na point 4 .

VIDEO YA TUKIO LA KUTAFUTA HIRIZI;

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox