STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 21 Septemba 2016

JOHN BOCCO NDIYE MCHEZAJI BORA WA MWEZI WA 8

MSHAMBULIAJI na nahodha wa Azam FC John Bocco amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Agosti kwa msimu wa 2016/2017.

Bocco  aliwashinda wachezaji Mzamiru Yasin wa Simba na Said Kipao wa JKT Ruvu. Katika mechi mbili ilizocheza katika mwezi huo, Bocco aliifungia  timu yake mabao matatu likiwemo la kusawazisha dhidi ya African Lyon.


 Bocco pia alifunga mabao mengine mawili kwenye ushindi wa mabao 3-0 wa timu yake dhidi ya Majimaji. Katika mechi hizo mbili, Azam FC ilifanikiwa kupata pointi nne kati ya sita.


Mwezi huo ulikuwa na raundi mbili tu za Ligi hiyo iliyoanza kutimua vumbi Agosti 20 mwaka huu. Kwa kushinda tuzo hiyo, Bocco atazawadiwa kitita cha sh. milioni moja kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox