Mshambuliaji wa klabu ya Simba Danny Lyanga amefuzu majaribio katika klabu ya Fanja ya nchini Oman na inaelezwa jana jioni alisaini mkata wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo.
Awali msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara alithibisha Lyanga alikwenda Oman kwa ajili ya kufanya majaribio katika klabu ya Oman Club lakini haikufahamika kama alifuzu au la na badala yake imetoka taarifa ya mchezaji huyo kusajiliwa Fanja.
Hadi Lyanga anaondoka Simba msimu huu alikuwa hajacheza mechi ya ligi, mchezo aliocheza ulikuwa ni wa kirafiki dhidi ya Polisi Dodoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni