WAZIRI wa Habari Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye amesema kwamba Serikali haina pingamizi kwa Simba kurejesha mechi zake Uwanja wa Taifa kutoka wa Uhuru, Dar es Salaam.
Na
Nape amesema kwamba wenye mamlaka ya kurejesha mechi za Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania za Simba Uwanja wa Taifa ni Bodi ya Ligi na Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF). “Sisi hatuna tatizo, wao wamalizane na Bodi ya
Ligi na TFF,”alisema Nape akizungumza jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Waziri Nape Nnauye (kushoto) akizungumza leo mjini Dar es Salaam |
Katibu wa Simba SC, Patrick Kahemele alisema juzi mjini Dar es Salaam kwamba wachezaji wao watatu waliumia katika mchezo uliopita wakishinda 1-0 dhidi ya Azam FC Jumamosi kutokana na ubaya wa eneo la kuchezea la Uwanja wa Uhuru.
“Vile vipira vya kwenye nyasi bandia pale uwanjani vimeharibika kutokana na kutotumika kwa muda mrefu, kwani vimepigwa jua, vimefubaa na kuwa kama vipande vya chupa, hivyo kuhatarisha usalama wa wachezaji wanapoanguka,”alisema Kahemele.
Katibu huyo pia akasema Uwanja wa Uhuru ni mdogo ambao hauendani na mahitaji ya soka ya kisasa na kwamba hawatakuwa tayari kuutumia tena hadi hapo utakapokaguliwa na kuidhinishwa a wakaguzi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
“Hatutaki na hatutoutumia Uwanja wa Uhuru hadi pale utakapofanyiwa marekebisha makubwa na kukaguliwa na wakaguzi wa CAF na FIFA,”alisema Meneja huyo wa zamani wa Azam FC.
Pamoja na kuulalamikia Uwanja wa Uhuru, Simba SC imeshinda mechi zake zote ilizocheza hapo dhidi ya Ruvu Shooting 2-1, Mtibwa Sugar 2-0 na Azam 2-0.
Katika mechi zake mbili za awali ilizocheza Uwanja wa Taifa, ilishinda moja 3-1 dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara na kutoa sare ya 0-0 na JKT Ruvu.
Baada ya barua hiyo, sasa linasubiriwa tamko la Bodi ya Ligi juu ya wapi mchezo ujao wa Simba SC dhidi ya Maji Maji ya Songea utachezwa.
STORI YA PILI;
TANZANIA Bara imefanikiwa kutwaa ubingwa wa kwanza wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kenya jioni ya leo Uwanja wa Ufundi, Jinja.
Shukraani
kwao, wafungaji wa mabao hayo, Mwanahamisi Omar ‘Gaucho’ na Stumai
Abdallah dhidi ya moja la Kenya, lililofungwa na Christine Nafula.
Kocha wa Kilimanjaro Queens, Sebastian Nkoma amefurahia ushindi huo na kuwapongeza wachezaji wake kwa kazi nzuri.
Wachezaji wa Kilimanjaro Queens wakisherehekea baada ya kukabidhiwa Kombe lao
Wachezaji wa Kilimanjaro Queens wakishangilia ushindi wao leo
“Nimefurahi sana kwa matokeo haya, napenda nichukue nafasi hii kuwapongeza wachezaji wangu kwa ushindi huu, tumedhihirisha ubora wetu hapa,”alisema Nkoma.
Ikumbukwe, Kilimanjaro Queens iliingia fainali baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya wenyeji, Uganda, wakati Kenya iliifunga 3-2 Ethiopia.
Awali, Tanzania Bara iliongoza Kundi B baada ya kushinda kura ya sarafu kufuatia sare ya 0-0 na Ethiopia katika mchezo wa mwisho wa kundi hilo, hivyo kufungana nayo kwa pointi na wasatani wa mabao kileleni.
Kilimanjaro Queens ilianza vizuri michuano hiyo kwa kuibamiza 3-2 Rwanda, mabao yake yakifungwa na Asha Rashid ‘Mwalala’ dakika za 11 na 65 na Stumai Abdallah dakika ya 28, wakati ya wapinzani wao yalifungwa na Ibangarrue Marie na Amina Ally wa Tanzania Bara aliyejifunga.
Kikosi cha Kilimanjaro Queens leo kilikuwa; Fatuma Omar, Donisia Daniel, Fatuma Bushiri, Amina Ally, Stumai Abdallha, Wema Richard, Maimuna Khamis, Anastazia Anthony, Fatuma Issa, Mwanahamisi Omar ‘Gaucho’ na Asha Rashid ‘Mwalala’.
Benchi; Belina Julius, Fadhila Hamad, Fatuma Hassan, Sherida Boniphace, Fatuma Mustafa na Anna Hebron.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni