BAO pekee la Shiza Ramadhani Kichuya limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kichuya alifunga bao hilo dakika ya 67 kwa shuti la kitaalamu baada ya kupokea pasi nzuri ya kiungo Said Hamisi Ndemla.
Kwa ushindi huo, Simba SC sasa inajinafasi kileleni mwa Ligi Kuu, ikifikisha pointi 13 baada ya mechi tano, ikifuatiwa na mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 10 sawa na Azam.
Shiza Kichuya akishangilia baada ya kuifungia Simba SC bao pekee leo
Winga Muivory Coast wa Azam FC, Ya Thomas Renardo akiwatoka mabeki wa Simba leo
Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Hajib akiwatoka mabeki wa Azam FC leo
Mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco akifumua shuti mbele ya beki wa Simba, Method Mwanjali
John Bocco akigombea mpira wa juu na beki wa Simba Novaty Lufunga
Simba SC walistahili ushindi katika mchezo wa leo kutokana na kupeleka mashambulizi mengi zaidi langoni mwa Azam FC.
Hata hivyo, umaliziaji haukuwa mzuri leo kwa Wekundu wa Msimbazi, kwani walipoteza nafasi kadhaa nzuri za kufunga tangu kipindi cha kwanza.
Nahodha wa Azam FC, John Bocco aliyekuwa mshambuliaji pekee leo alijitahidi lakini hakuweza kufurukuta mbele ya mabeki wa Simba SC, Novaty Lufunga na Mzimbabwe Method Mwanjali.
Ibrahim Hajib alikuwa tishio zaidi kwenye safu ya ulinzi ya Azam FC, lakini hakuweza tu kufunga, wakati Mrundi Laudit Mavugo hakufurukuta kabisa na akatolewa kipindi cha pili Muicory Coast, Frederick Blagnon aliyekwenda kukosa bao la wazi.
Ushindi huo ni faraja kwa kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog kwani ameifunga timu yake ya zamani, Azam FC iliyomfukuza mwaka jana.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa: Aishi Manula, Shomary Kapombe, Bruce Kangwa, David Mwantika, Jean Baptiste Mugiraneza, Himid Mao, Frank Domayo/Mudathir Yahya dk76, Salum Abubakar ‘Sure Boy’,Ya Thomas Renardo, John Bocco na Khamis Mcha ‘Vialli’/Francesco Zekumbawira dk76.
Simba: Vincent Angban, Janvier Besala Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga, Method Mwanjali, Shiza Kichuya/Mohamed Ibrahim dk, Muzamil Yassin, Laudit Mavugo/Frederick Blagnon dk, Jonas Mkude, Ibrahim Hajib na Jamal Mnyate/Said Ndemla dk63.
WAKATI HUO;
Beki wa kushoto wa Simba, Mohammed Hussein maarufu kwa jina la Tshabalala au Zimbwe Jr ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Simba kwa mwezi Agosti, 2016.
Zimbwe Jr ambaye katika siku za hivi karibuni na hata katika msimu uliopita amekuwa nguzo muhimu katika kikosi cha Simba, alikabidhiwa tuzo hiyo leo Jumamosi kabla ya mchezo wa Simba dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Uhuru ambao timu yake ilishinda bao 1-0.
Zimbwe alikabidhiwa tuzo yake hiyo uwanjani hapo na Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba, Geophrey Nyange 'Kaburu' pamoja na Mkurugenzi wa EAG Group, Imani Kajula.
Makabidhiano ya tuzo hiyo yalienda sambamba na zawadi ya fedha shilingi 500,000.
Licha ya kuwa na namba ya uhakika katika kikosi cha kwanza cha Simba, Zimbwe pia amekuwa akipata nafasi katika kikosi cha TaifA Stars.
VIWANJA VINGINE;
Mabingwa
Watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga wamefanikiwa kuibuka na
ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Matajiri wa Almasi timu ya Mwadui FC,
mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Katika
mchezo huo uliotawaliwa na ubabe wa hapa na pale, Yanga waliuanza
mchezo kwa kasi na ndipo mnamo dakika ya sita tu, mshambuaji hatari wa
timu hiyo Amissi Tambwe alipofunga bao la uongozi kufuatia mpira kuzagaa
zagaa langoni mwa timu ya Mwadui kutokana na mpira wa faulo uliochingwa
na Juma Abdul.
Amanusura Yanga wapate bao la pili dakika ya 12 lakini shuti la Donald Ngoma liligonga mwamba na kutoka nje.
Msuva alikaribia kufunga goli dakika ya 15 na 20 lakini umakini mdogo ulimfanya ashindwe kufunga.
Dakika ya 43, kiungo mahiri wa Yanga Thabani Kamusoko aliumia na nafasi yake kuchukuliwa na Haruna Niyonzima.
Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa Yanga kuwa mbele kwa bao 1-0.
Takwimu za kipindi cha kwanza
Dakika
ya 81 Msuva kwa mara nyingine tena alishindwa kufunga goli la wazi
baada ya shuti lake kudakwa kwa umahiri mkubwa na kipa wa Mwadui.
Yanga
walipata pigo lingine baada ya mchezaji wao mwingine beki Kelvin Yondan
kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Nadir Haroub Ally 'Cannavaro'.
Mshambuliaji
wa Yanga kutoka Zimbambwe Donald Dombo Ngoma aliifunga goli la pili
dakika ya 90 na kuzima ndoto za Mwadui kurudisha goli walau kupata sare
katika uwanja wao wa Nyumbani.
Hii ni mara ya tatu Yanga na Mwadui wanakutana. Yanga wamefanikiwa kushinda mara mbili na kutoka sare mara moja.
FT
|
MBEYA CITY
|
0
|
:
|
0
|
T.PRISONS
|
FT
|
MTIBWA SUGAR
|
2
|
:
|
0
|
KAGERA SUGAR
|
FT |
RUVU SHOOTING
|
1
|
:
|
4 |
MBAO FC
|
FT |
MAJIMAJI
|
1
|
:
|
2
|
NDANDA FC
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni