STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 17 Septemba 2016

''CHUNGU LAKINI NI DAWA KATIKA SOKA LETU.........''

 Tokeo la picha la muarubaini

''Acha nikwambie,manake nisipokwambia hautoweza kuamini''.

Tokeo la picha la tff TANZANIA 


Wikend iliyomallizika nikiwa sehemu moja hivi kwenye kibanda umiza nikifuatilia mechi ya ligi kuu Tanzania bara kati ya Yanga na Majimaji nikiwa sina hili wala lile, ndipo rafiki yangu Philipo Darely akanishtua kidogo.

''Aaaah nilishtuka kweli''.


Alikuja akaniuma sikio akaniambia,hivi watanzania si bado tupo kwenye maombolezo?


Nikajibu harakaharaka,ndiyo ni kifo cha mkongwe wetu mzee Mohammed msomali.


Tokeo la picha la MOHAMED MSOMALI 

Aliniambia,kwa kumpoteza mzee wetu katika medani ya soka lazima tuelendelee kuomboleza.

Akatikisa kichwa kuashiria alikuwa anasikitika kwa muda sikuwa namuelewa sana alichokuwa ananiambia kwa sababu mawazo yangu yalikuwa kumuona kamusoko na rasta zake huku akipiga zilee pasi zake.


Nilitaka kuendelea kufaidi kumwona ngoma akiwanyanyasa mabeki Lakini rafiki yangu huyu alitaka nimwelewe alichokuwa anakimaanisha.


Aliniambia sikia embu kuwa makini na kile ninacho kujuza ,ujue watanzania tumekuwa tukiishi katika nyakati tofauti na wanazoishi wenzetu.


Nilikuwa nimetega sikio langu kwa uzuri kabisa kumsikiliza.
Yanga na Majimaji wanacheza katika kipindi hiki cha maombolezo,lakini katika mchezo huu hakuna kiashiria chochote kile kinachoonesha wapo katika maombolezo ya kuondokewa na legendary wa soka la Tanzania mzee Mohammed msomali.


''Wanaona sawa tu hawataki kumpa heshima yake''


 Ooooh ama kweli jamaa alinitoa tongotongo kwelikweli.
Nikafanikiwa kufumbua macho yangu kwa umakini hapohapo nikaanza kuvuta picha hali ya kabla ya mchezo.


Mhhh vipi,yanga na majimaji  walisimama kweli hata nusu dakika kwa ajili ya heshima kwa msomali?


''Hapana hawakusimama.''


Nikaona kama hawakusimama ngoja niangalie hata vile vitambaa vyeusi kwenye mikono yao,sikufanikiwa kuviona.


Hapohapo nikaona sura ya rafiki yangu ikiwa ya huzuni kabisa.
Aliumia sana kwa hali ile.


Hata mimi nikajikuta naumia pia hakikuwa kitendo cha heshima hata kidogo kwa mzee wetu msomali.


Nikajiuliza kwa sasa tunamfikiriaje huyu mzee?
au ndo aliyekufa kafa.


Nikaona labda yanga na majimaji huenda wakawa wamesahau kama tupo kwenye maombolezo.


Nikaona ngoja niwasubiri watani zao simba ambao kesho yake wangekuwa uwanjani kupambana na mtibwa.


Nikawahi siti ya mbele kabisa kesho yake ili nione kwa ukaribu zaidi.
Ooooh mambo yakawa ni yaleyale niliyoyaona jana yake nilishtuka sana kwa nilichokiona.


Hapo ndipo nikagundua heshima za malegendary wetu kama kina Msomali zimejaa mdomoni na siyo moyoni.


Nikajiuliza yani hata TFF wameshindwa kuviongoza vilabu katika hili.


Mhhh kwani kusimama dakika moja kwaajili ya kutoa heshima kwa msomali wangetozwa shilingi ngapi?


Anhaaaa labda mawazo yao yaliwatuma kuwa aliyekufa kafa.
Jamani lakini mbona ni majibu mepesi sana katika maswali magumu kama haya.


Nikaona nikumbuke mbali kidogo nikavuka mipaka na kuikumbuka  ile siku Newcastle united,Chelsea, man united,kina Liverpool, arsenal na wengine waliposimama dakika moja moja katika mechi zao kwaajili ya kutoa heshima kwa Gary speed.


 Tokeo la picha la NEWCASTLE RESPECT ON GARY SPEED  DEATH

Nikakumbuka heshima iliyotolewa kwa kifo cha yohan Cruyff. Nikakumbuka hata heshima iliyotolewa kutokana na ule mlipuko wa kule ufaransa.
 Tokeo la picha la BARCELONA RESPECT ON JOHAN CRUFF DEATH

Nikajiridhisha kuwa wenzetu wako makini katika hili.

Aaah sasa mbona sisi ni tofauti?


Kama tumeshindwa kwa mtu wa soka mwenzetu  hivi tutawezaje kwa wale watu wa bukoba ambao hatujui hata wanachokipenda?


Naingoja weekend hii kuona tunaomboleza vifo vya watu wa bukoba kama itashindikana ntajiaminisha kuwa bado tunaishi maisha yetu wenyewe kwenye dunia yetu.

Naingoja kwa hamu kweli siku hii.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox