STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 15 Septemba 2016

MATOKEO NA REKODI ZA MECHI ZA JANA UEFA CHAMPIONS LEAGUE......

Real Madrid leave it late, Leicester and Dortmund cruise

Nyota wa Ureno, Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia bao la kusawazisha Real Madrid dakika ya 89 kabla ya Alvaro Morata kufunga la pili dakika ya nne ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika ya 90 katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Sporting Lisbon ya Ureno usiku wa jana Uwanja wa Bernabeu kwenye mchezo wa Kundi F Ligi ya Mabingwa Ulaya.



 Sporting Lisbon ilitangulia kwa bao la Bruno Cesar dakika ya 47. Mchezo mwingine wa kundi hilo, Borussia Dortmund iliwafunga wenyeji, Legia Warszawa mabao 6-0 




Ronaldo alioongeza rekodi yake ya kushindwa kufunga free-kick ya 43 kwenye michuano mikubwa akiwa na Ureno kwenye michuano ya Euro mwaka huu, lakini ameondoa mkosi huo jana kwa kufunga faulo nzuri aliyopiga kutoka takriban umbali wa hatua 25.

Goli hili alililofunga ni la 12 kwa njia ya free-kick tangu aanze kucheza michuano hiyo huku akiwa na rekodi ya kufunga jumla ya mabao 94 kwenye mashindano huku magoli 79 katika michezo 76 akifunga akiwa kama mchezaji wa Real.

Ronaldo sasa anakuwa mchezaji ambaye amefunga kwenye kila mchezo kati ya mitano ambayo alikutana na timu yake ya nyumbani kwenye Michuano ya Champions League.

Alifunga nyumbani na ugenini dhidi ya Sporting wakati akiwa Manchester United mwaka 2007, na alifunga kwenye mechi zote mbili kwenye hatua ya robo fainali fainali ya mwaka 2013 wakati Real Madrid akicheza na MMan United.

.....................

Ryad Mahrez (kulia) akishangilia na wenzake baada ya kuifungia kwa penalti Leicester City dakika ya 61 hilo likiwa bao lake la pili usiku wa jana baada ya awali kufunga dakika ya 29 katika ushindi wa 3-0 dhidi ya wenyeji, Club Brugge kwenye mchezo wa Kundi G Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Jan Breydel mjini Brugge.

 Bao lingine la Leicester lilifungwa na Marc Albrighton dakika ya tano .

........................


Nyota wa Argentina, Sergio Aguero akishangilia baada ya kuifungia Manchester City mabao matatu peke yake katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Borussia Monchengladbach katika mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Etihad. 

Bao lingine la City lilifungwa na Kelechi Iheanacho.

...............


Tottenham Hotspurs wamefungua vibaya pazia la Michuano Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufungwa na Monaco ya Ufaransa mabao 2-1.

Wakicheza Wembley ambapo wanatumia kama uwanja wao wa nyumbani kwenye michuano hii, Spurs walijikuta wakiruhusu bao la mapema kabisa dakika ya 16 lilikofungwa na Bernardo Silva.

Monaco waliongeza bao la pili mnamo dakika ya 31 lililofungwa na Bernardo Silva.

Spurs walifanikiwa kupata goli lao pekee katika mchezo huo lililofungwa dakika ya 45 kupitia kwa Toby Alderweireld.

.......................

MATOKEO YOTE KWA UJUMLA;


....................

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox