Manchester United wametoa kipigo cha mbwa mwizi dhidi ya Mabingwa Watetezi wa Premier League Leicester City kwa kwafunga mabao 4-1, mchezo uliofanyika kunako Uwanja wa Old Trafford.
Katika
mchezo huo ambao nahodha wa United Wayne Rooney alianzia benchi, Man
United walipata bao la kwanza dakika ya 22 kupitia kwa Chris Smalling
kuunganisha mpira wa kona uliopigwa na Daley Blind.
United
waliongeza bao la pili kupitia kwa Juan Mata dakika ya 37 baada ya
kugongeana pasi kwa uzuri na Lingard kuwahadaa mabeki wa Leicester.
Bao la tatu la United lilifungwa na Marcus Rashford dakika ya 40 baada ya kuunganisha pasi nzuri ya Juan Mata.
United walifunga bao lao la mwisho dakika ya 42 kupitia kwa Pogba kufuatia kona nzuri iliyochongwa na Daley Blind.
Leicester City walipata bao pekee la kufutia machozi dakika ya 60 kupitia kwa juhudi binafsi za Demarai Gray.
Nahodha wa United Wayne Rooney aliingia dakika ya 83 kuchukua nafasi ya Marcus Rashford.
Mtu
mmoja ambaye anafanana na Zlatan Ibrahimovic ameibuka uwanjani kwa
kuwalaghai walinzi na kwenda hadi alipokuwa Zlatan mwenyewe wakati
akiitumikia timu yake dhidi ya Leicester City.
Mtu huyo alifanikiwa kumvaa Zlatan na kusababisha watu kuangua kicheko wakiwemo wachezaji wa Man United waliokuwa benchi.
TAARIFA YA PILI;
SIMBA
SC imezidi kutanua kwapa kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada
ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Maji Maji ya Songea jioni ya leo Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo uliotokana na mabao ya Jamal Simba Mnyate mawili na moja la Shizza Ramadhani Kichuya, unaifanya Simba SC ifikishe pointi 16, baada ya kucheza mechi sita, wakishinda tano na sare moja.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na Ludovic Charles wa Tabora aliyesaidiwa na Anord Bugando wa Singida na Joseph Masija wa Mwanza, hadi mapumziko Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Bao
hilo lilifungwa na kiungo mpya, Jamal SImba Mnyate aliyesajiliwa kutoka Mwadui
FC ya Shinyanga dakika ya nne akimalizia mpira uliotemwa na kipa Aman Simba
baada ya shuti la Ibrahm Hajib aliyeunganisha krosi ya Laudit Mavugo.
Simba ikapata pigo dakika ya 21 baada ya mshambuliaji wake tegemeo, Ibrahm Hajib kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na kiungo Said Ndemla.
Shizza Ramadhani Kichuya akaifungia Simba SC bao la pili kwa penalti dakika ya 67 baada ya beki wa Maji Maji, Lulanga Mapunda kuunawa mpira kwenye boksi.
Mnyate akawainua tena wapenzi wa SImba vitini kwa kufunga bao la tatu dakika ya 74 akimalizia krosi ya Mo Ibrahim.
Kichuya akakamilisha sherehe za mabao za Simba SC kwa kufunga la nne dakika ya 81 baada ya kumlamba chenga kipa mkongwe wa Maji maji, Amani Simba baada ya pasi ndefu ya Nahodha Jonas Gerald Mkude.
Baada ya ushindi huo, Simba inakwenda kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu wao, Yanga SC Jumamosi wiki ijayo Uwanja huo huo wa Taifa.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Vincent Angban, Janvier Besala Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shizza Kichuya, Muzamil Yassin/Mohammed ‘Mo’ Ibrahim dk51, Laudit Mavugo/Ame Ali dk62, Ibrahim Hajib/Said Ndemla dk21 na Jamal Mnyate.
Maji Maji; Amani Simba, Suleiman Kibuta/Tarik Simba dk80, Bahati Yussuf, Hamad Kibopile, Ernest Raphael, Lulanga Mapunda, Alex Kondo, Luka Kikoti/Marcel Boniventura dk59, Darlington Enyina, George Mpole na Paul Maona.
MATOKEO MENGINE;
JKT RUVU
|
2
|
:
|
0
|
MBEYA CITY
|
|
NDANDA FC
|
2
|
:
|
1
|
Azam FC
|
|
T.PRISONS
|
0
|
:
|
0
|
MWADUI FC
|
|
MTIBWA SUGAR
|
1
|
:
|
1
|
MBAO FC
|
MICHEZO INAYOKUJA;
2016-09-25
16:00 | RUVU SHOOTING | Vs | TOTO AFRICANS |
16:00 | STAND UNITED | Vs | YANGA |
TAARIFA YA TATU;
Timu
ya Mpira wa Miguu ya Tanzania (Taifa Stars), inatarajiwa kucheza na
Ethiopia katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa Oktoba 8, 2016.
Mchezo
huo utakaofanyika jijini Addis Ababa, umeratibiwa kwa mujibu wa kalenda
ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo huwa na
kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa kwa wanachama wake – Tanzania ni
miongoni mwao. Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ethiopia (EFF), wameomba
mchezo huo ufanyike kwao.
Hii ni faida kwa Tanzania kama itashinda mchezo huo kwa maana kina alama za nyongeza kama inatokea unaifunga timu mwenyeji.
Kocha
Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa atakuwa na nafasi ya
kuandaa kikosi chake kuanzia Oktoba 3, 2016 mara baada ya michezo ya
Ligi Kuu Tanzania Bara ambako Mwadui itacheza na Azam huku Mbao
ikishindina na JKT Ruvu Oktoba 2, mwaka huu kabla ya kupisha kalenda
hiyo ya FIFA ya michuano ya kimataifa.
Matokeo
ya mchezo huo, ni sehemu malumu kupima viwango vya ubora na uwezo wa
timu za taifa. Kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya 132 kati ya nchi 205
wanachama wa FIFA zilizopimwa ubora. Ethiopia yenyewe inashika nafasi
ya 126.
Argentina
inaongoza ikifuatiwa na Ubelgiji anakocheza Mbwana Samatta – nyota wa
kimataifa wa Tanzania. Samatta anacheza klabu ya K.R.C Genk inayoshiriki
Ligi Kuu ya Ubelgiji. Timu nyingine bora kimataifa ni Ujerumani,
Colombia na Brazil.
Katika
Bara la Afrika, Ivory Coast ambayo ni ya 34 kwa ubora duniani ndiyo
inayoongoza ikifuatiwa na Algeria, Senegal, Tunisia na Ghana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni