TAARIFA YA KWANZA;
Cristiano
Ronaldo ameonesha kitendo cha utovu wa nidhamu mbele ya kocha wake
Zinedine Zidane pale alipofanya uamuzi wa kumpumzisha mshindi huyo wa
Champions League na European Championship wakati wa game dhidi ya Las
Palmas.
Ronaldo alikunja sura kuonesha kuchukizwa na maamuzi ya Zidane kuhusu kumpumzisha.
Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Ronaldo kupumzishwa kwa sababu za kiufundi wakati wa mchezo mgumu.
Wakati
Ronaldo anapumzishwa dakika ya 72, Real Madrid ilikuwa inaongoza kwa
2-1 mbele ya Las Palmas. Zikiwa zimesalia dakika 5 mechi kumalizika, Las
Palmas wakasawazisha kwa goli la Sergio Araujo.
Mwisho
wa mchezo, Real Madrid ikapoteza pointi mbili wakati ilikuwa ikipambana
kurejea kileleni mwa La Liga baada ya Barcelona kushinda 5-0 kwenye
mechi yao ya mchana.
BAADA YA RONALDO KUONESHA VITENDO VISIVYO VYA KIMICHEZO BAADA YA KUFANYIWA SUB NA ZIDANE, HAYA NDIYO YALIYOJIRI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII;
TAARIFA YA PILI;
WALICHOKIANDIKA MASHABIKI WA CHELSEA JUU YA ANTONIO CONTE BAADA YA KIPIGO CHA 3-0 KUTOKA KWA ARSENAL
Didier
Drogba kwa sasa hawezi tena kuidhuru Arsenal uwanjani, lakini bado
anaweza kuwafanyia hivyo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kumpa
kijembe Theo Walcott kupitia Twitter.
Walcott
ameendelea kuwa kwenye kiwango bora tangu msimu mpya kuanza baada ya
kufunga goli moja kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya mahasimu wao
Chelsea.
Baada ya mchezo huo alionesha furaha kubwa juu ya matokeo hayo na kupost picha akiwa anasherehekea iliyoambatana na ujumbe.
Hata hivyo, kupitia tweet hiyo Drogba alimjibu Walcott kwa kumpongeza kwa ushindi na kurusha kijembe cha utani kiaina.
Drogba
aiandika hivi: 'Hongera sana kwa ushindi bro @theowalcott, lakini ni
rahisi sana kwa panya kutawala pale paka anapokuwa hayupo'.
Drogba
anakumbukwa kwa kuwa mwiba mkali kwa Arsenal wakati akicheza Chelsea
kila walipokutana, akiwa amefunga magoli 15 kwenye michezo 16 kati ya
mwaka 2004 na 2012.
Na
hivi karibuni tena aliwafunga Arsenal kwa mara nyingine kwenye mchezo
wa kirafiki wa pre-uliofanyika Marekani, ambapo alikuwa miongoni mwa
wachezaji waliounda kikosi cha MLS All-Stars kilichofungwa mabao 3-1.
Kabla
ya mchezo wa jana katika dimba la Emirates, Arsenal walikuwa
wamewafunga Chelsea mara moja ndani ya miaka mitano. Hiyo ilikuwa mwaka
2011 wakati huo Cesc Fabregas alikuwa nahodha wa Arsenal.
TAARIFA YA TATU;
WANAYANGA MMEMSIKIA HAJI MANARA!!
Ushindi
wa mabao 4-0 dhidi ya Majimaji umempa kiburi Mkuu wa Kitengo cha Habari
na Mawasiliano cha Simba Haji Manara na kusema moto wao hauzimiki mpaka
mwisho wa msimu.
Manara
amesema msimu huu Simba haidharau timu timu yeyote kwenye ligi huku
akisisitiza timu yake imejipanga kuongoza ligi kudumu hadi mwisho.
“Macho
yetu na masikio yetu tunaelekeza October 1, ni mechi ya kawaida kama
mechi nyingine ya ligi na hatuipi u-special wowote ule. U-special wake
ni kwasababu ya kucharuana kwa mashabiki lakini uzito ni ulele tulioutoa
kwenye mechi ya Majimaji ndio tutautoa ligi nzima hatutadharau timu
yeyote”, amesema Manara mara baada ya mechi kati ya Simba dhidi ya
Majimaji.
“Tutacheza
na Yanga kama tunacheza na mkubwa mwenzetu, hatujali hii ni timu ndogo
au kubwa tunatakiwa tuongoze ligi kwa kudumu hadi ligi inamalizika.”
“Hatutadharau
mechi inayokuja, mechi ya leo ni sawa na mechi inayokuja bila kujali ni
Yanga au timu nyingine yeyeyote, kila mechi ni fainali hiyo ndiyo
kaulimbiu ya Simba msimu huu.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni