YANGA YATOKOTA MBELE YA STAND KAMBARAGE
Stand
United ‘Chama la Wana’ wamevunja rekodi ya Yanga baada ya kuifunga bao
1-0 kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa uwanja wa CCM
Kambarage mkoani Shinyanga.
Bao pekee la Stand limefungwa na Pastore Athanasi ambalo limeifanta tumu take iibuke na pointi tatu kwenye uwanja wa nyumbani.
Licha
ya Stand kuwa kwenye mpasuko mkubwa wa kiutawala, timu hiyo bado
haijapoteza mchezo wowote kwenye uwanja wao wa nyumbani hadi sasa tangu
kuanza kwa ligi mzimu huu 2016-2017.
Rekodi za Yanga zilizo unjwa na Stand United
- Stand United imeifunga Yanga kwa mara ya kwanza tangu timu hiyo ya Shinyanga mjini ilipopanda daraja.
- Yanga imepoteza mchezo wake wa kwanza wa VPL msimu baada ya kucheza mechi nne bila kufungwa.
- Stand United imekuwa timu ya kwanza kufunga goli dhidi ya Yanga. Awali Yanga ilikuwa imecheza mechi nne za ligi bila kuruhu goli huku yenyewe ikiwa imefunga magoli nane.
- TAARIFA YA PILI;
-
- WABUNGE wanaoshabikia
timu ya Yanga wamewabugiza wenzao wa Simba kwa mabao 5-2 kwenye mchezo
wa hisani kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera
uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo ambao Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa alikuwa mgeni rasmi, Yanga walionekana kuwazidi Simba karibuni kila idara ambapo Ridhiwani Kikwete ya Yanga alikuwa mwiba mkali.
Sadifa Hamisi aliipatia Yanga bao la kwanza dakika ya tatu kabla ya Mohamed Mchengerisa hajafunga mabao mawili ya haraka dakika ya 5 na 8.
Cosato Chami aliifungia Simba bao la kwanza dakika ya 18 kabla ya Mwigulu Nchemba kuongeza mabao ya haraka kwa Yanga dakika ya 25 na 28.
Kaiza Makame aliipatia Simba bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 39 baada ya mchezaji mmoja wa Wekundu hao kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari.
Matokeo mengine Wasanii wa Bongo fleva waliwafunga Bongo Bovies kwa changamoto ya mikwaju ya penati 5-4 baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 katika muda wa kawaida.
Bongo Movies ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 11 kupitia kwa Nteze kabla ya H baba kusawazisha dakika ya 17.
Kwa upande wa Netball timu ya Wabunge Wanawake waliwafunga TBC vikapu 15 -14.
Mapato yaliyopatikana ni sh 187 milioni 187 ambapo pesa zote zitapelekwa kwa wahanga kama ilivyopangwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni