SHIRIKISHO la mpira wa
miguu Tanzania TFF limetangaza viingilio vya mchezo wa 'Watani wa Jadi' Simba
na Yanga wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara utakaofanyika kwenye uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam Jumamosi Octoba mosi.
Simba inakutana na watani wao wakiwa vinara wa ligi baada ya kushinda Michezo mitano na kutoka sare mmoja huku Yanga wakishinda minne, kutoka sare mmoja na kupoteza mmoja.
Afisa Habari wa TFF Alfred Lucas amevitaja viingilio hivyo kuwa VIP A ni sh 30,000 VIP B & C sh 20,000 na mzunguko utakuwa sh 7,000.
Mashabiki watakaotaka kushuhudia mtanange huo uwanjani watatakiwa kutumia tiketi za Kielectoniki ambazo ndiyo pekee zitakazowezesha kuutazama mchezo huo ambao unaziba mianya yote ya kuingia bila kulipa.

Kwa upande wake Mkurugenzi
wa kampuni ya Selecom ambao ndiyo wasimamizi wa tiketi hizo Galus Runyeta
alisema tiketi hizo zitaanza kuuzwa kuanzia kesho katika vituo mbali mbali
jijini hapa.
Baadhi ya vituo hivyo ni Vituo vya mafuta vya Total, Village Supermarket, Vituo vya mafuta ya Puma, Samaki Samaki, Buguruni Sheli, Mlimani City, Sinza Africa Sana na Uwanja wa Taifa.
Aidha Galus amewataka mashabiki wa timu hizo kununua tiketi mapema kuanzia kesho katika vituo tajwa ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza siku ya mtanange huo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni