YANGA SC imewasilisha barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupinga klabu ya Stand United kumtumia mchezaji Frank Khamis Igobela katika mchezo wa Jumapili.
Yanga ilifungwa 1-0 na Stand United Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Kambarage, Shinyanga na baada ya mchezo ikawasilisha rufaa.
Yanga inadai Stand United imemtumia Igobela kimakosa kwa kuwa bado ni mchezaji halali wa Polisi ya Zanzibar.
Chanzo cha habari kutoka Yanga SC kimesema kwamba, klabu imepata taarifa za kutosha kutoka Polisi ya Zanzibar juu ya mchezaji huyo.
Na Yanga wanadai kwamba wana ushahidi hadi wa barua ya Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kikiizuia TFF kumuidhinisha mchezaji huyo kucheza Ligi Kuu hadi amalizane na Polisi.
Na Yanga wanadai wanaamini Igobela alicheza mechi ya Jumapili akiwa hana leseni, lakini wamejaribu kufuatilia TFF tangu jana hawajapata majibu.
..................
STORI YA PILI;
Martin Saanya ameteuliwa kuchezesha mchezo baina ya watani wa jadi, Simba na Yanga Jumamosi wiki hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Saanya mwenye beji ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), alifungiwa mwaka mmoja na uongozi uliopita wa TFF, chini ya Rais Leodegar Tenga kwa tuhuma za kuvurunda mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Yanga na Coastal Union iliyomalizika kwa sare ya 1-1 msimu wa 2013/14.
Saanya akimdhibiti mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbangu (kushoto) asipigane na beki wa Simba SC, Nassor Masoud 'Chollo' (kulia) mbele ya kocha wake, Mfaransa, Patrick Liewig
Lakini, chini ya uongozi mpya wa TFF wa Rais Jamal Malinzi, Sanya akafutiwa adhabu na kuendelea na kazi – na Jumamosi atachezesha mchezo mwingine mkubwa wa Ligi Kuu baina ya watani, Simba na Yanga.
Mara ya mwisho Saanya kuchezesha mechi kubwa ilikuwa msimu uliopita alipopuliza kipyenga kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii, Yanga ikiifuga Azam.
Lakini pia hii si mara ya kwanza kwa Saanya kuchezesha mechi ya watani, kwani msimu wa 2013/2014 alichezesha mchezo ambao Yanga ilishinda 2-0 mabao ya Hamisi Kiiza na Didier kavumbangu.
Katika mchezo huo, Saanya aliumia jicho wakati akiamulia ugomvi baina ya waliokuwa wachezaji wa timu hizo, mshambuliaji Mrundi wa Yanga, Didier Kavumbangu na beki Mzanzibari wa Simba SC, Nassor Masoud 'Chollo' na kutibiwa kwa dakika tatu.
Na katika mchezo wa Jumamosi, Saanya atasaidiwa na Samwel Mpenzu na Ferdinand Chacha.
Viingilio katika mchezo huo vinatarajiwa kuwa Sh 7,000, 10,000, 20,000 na 30,000.
Yanga imeweka kambi kisiwani Pemba na Simba ipo Morogoro kujiandaa na mchezo huo.
STORI YA TATU;
MATOKEO YA MICHEZO YOTE YA UEFA JANA ;
STORI YA NNE;
SAM ALLARDYCE ABWAGA MANYANGA ENGLAND;
Zikiwa
zimepita siku 67 tangu abebe majukumu ya kuinoa England, Sam Allardyce
kwa ridhaa yake ameamua kujuzulu nafasi yake ya umeneja kufuatia shutuma
nzito za kuonekana kwenye video akitoa ushauri wa jinsi wa kupindisha
sheria za usajili za FA, imethibitishwa.
Baada
ya uamuzi huo, bosi wa kikosi cha England cha chini ya miaka 21 Gareth
Southgate atashikilia wadhifa huo kwa muda na kuiongoza timu hiyo kwenye
michezo minne ijayo, michezo wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia dhidi
ya Malta, Slovenia na Scotland, na ule wa kirafiki dhidi ya Uhispania.
Mtandao
wa The Daily Telegraph lilichapisha kipande cha video kilichodaiwa
kumwonesha Allardyce akiwaambia watu wawili ambao wanahisiwa kuwa ni
kutoka Mashariki ya Mbali kwamba angewapa mbinu ya kupindisha sheria za
usajili wa wachezaji za FA kwa kutumia njia ya 'third-party ownership'.
Ametuhumiwa kufikia makubaliano ya kulipwa kiasi cha euro 400,000 ili kuwasaidia katika mchakato huo wa uvunjaji sheria na kuahidi kuwawaklisha katika baadhi ya matukio ambayo yangehodhiwa na FA.
Allardyce ,61, pia ametuhumiwa kumkosoa mtangulizi wake kwenye kiti cha umeneja wa England Roy Hodgson na msaidizi wake Gary Neville kufuatia England kutolewa na Iceland kwenye Michuano ya Euro 2016, huku akishindilia msumari mwingine kwa kusema kitendo cha FA kutumia gharama kubwa kuufanyia marekebisho Uwanja wa Wembley ni "upuuzi".
Allardyce anazidi kuhas England manager's disease
"FA inathibitisha kwamba Sam Allardyce ameacha nafasi yake kama meneja wa England," taarifa rasmi ya FA imeeleza.
"Kitendo alichokifanya Allardyce, kama ilivyoripotiwa leo, hakikuwa cha kiungwana hasa kwa meneja wa England. Amekubali kwamba amefanya kosa kubwa na tayari ameomba radhi. Hta hivyo kutokana na ukubwa wa shutuma, kwa pamoja FA na Allardyce wameamua kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba mara moja.
"Huu si umamuzi ambao umechukuliwa kijuu-juu isipokuwa baada ya kufikiria kwa kina ili kulinda maslahi mapana ya mchezo wa soka na kuendelea kuufanya mchezo kuendelea kuwa na heshima kubwa.
"Meneja wa timu ya England ya wakubwa lazima adumishe misingi imara ya nidhamu na kuonesha heshima katika mchezo wa soka kwa nyakati zote.
"Gareth Southgate atachukua nafasi hiyo na kusimamia michezo ijayo dhidi ya Malta, Slovenia, Scotland na Uhispania wakati huo FA ikianza mchakato wa kusaka kocha mpya.
"FA inapenda kumtakia Sam kila la heri kwa siku zijazo."

WARAKA WA SAM ALLARDYCE BAADA YA KUJIUZULU TIMU YA ENGLAND;
"Ilikuwa ni heshima kubwa kwangu kuteuliwa kuwa meneja wa England mwezi July na kwa hakika nimesikitishwa sana na jambo hili.
"Jioni ya leo (jana), nimekutana na Greg Clarke na Martin Glenn na kueleza azma yangu ya kuomba msamaha kwa tukio lililotokea."
"Japokuwa
nimeweka wazi kwenye yale mazungumzo yaliyorekodiwa kwamba maafikiano
yale yangehitaji uthibitisho ama kupitishwa na FA, lakini natambua
nimetoa baadhia ya kauli ambazo zimeumiza watu," Allardyce amezidi
kuelezea.
"Nikiwa
kama moja ya watu waliohudhuria kikao cha leo (jana), niliambiwa nitoe
ufafanuzi juu ya nilichokieleza na eneo ambalo mazungumzo hayo
yalifanyika. Na nimetoa ushirikiano mkubwa sana kwenye suala hilo.
"Vilvile najutia sana kauli zangu hasa kwa kumlenga mtu mmoja-mmoja."
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni