TAARIFA YA KWANZA;
NDUMBA HIZI ZIMEIBULIWA UWANJA WA TAIFA KUELEKEA DERBY YA YANGA NA SIMBA KESHO;
Vitu
ambavyo vinahisiwa kuwa na uhusiano na mambo ya kishirikiana ambavyo
baadhi ya mashabiki kati ya Yanga na Simba wamedaiwa kuvinasa kwenye
Uwanja wa Taifa kuelekea derby yao kesho.
Vitendo hivi ya kishrikina si vigeni sana kwenye mechi nyingi za Yanga na Simba.
VIBONZO KUELEKEA MCHEZO WA SIMBA DHIDI YA YANGA OCTOBER MOSI;
TAARIFA YA PILI;
TAARIFA MPYA KUTOKA YANGA KUHUSU SUALA LA JEZI MPYA YA KLABU
TAARIFA YA JEZI FEKI ZA YANGA;
Uongozi
wa Yanga unapenda kuwatangazia wanachama, mashabiki na wapenzi kuwa
klabu bado haijatoa jezi rasmi za kuvaliwa na wapenzi wake zenye nembo
ya mdhamini mpya wa Yanga.
Kuna
taarifa za uwepo wa jezi feki mitaani zenye nembo ya Yanga pamoja na
mdhamini mkuu tunatoa TAHADHARI kwa wapenzi wa Yanga kutonunua jezi hizo
mana zinatengenezwa kwa Lengo la kuhujumu mapato ya klabu.
Tumeshatoa
taarifa kwenye mamlaka husika ikiwemo jeshi la polisi na endapo mtu
atakutwa amevaa hiyo jezi atawajibikia kuisaidia polisi katika
uchunguzi.
Klabu itatoa taarifa sahihi ya lini jezi zake rasmi zitaanza kuwa mitaani.
Epuka kununua kisicho halali cha Yanga.
Imetolewa na idara ya habari na mawasiliano Yanga.
30/09/2016.
TAARIFA YA TATU;
WACHEZAJI WA GHANA HAWANA NGUVU KWA SABABU YA KUENDEKEZA NGONO
MKURUGENZI
wa Ufundi wa klabu ya Asante Kotoko, Malik Jabir amesema wachezaji wa
Ligi Kuu ya Ghana wanakosa nguvu kwa sababu wanapenda sana ngono.
Jabir ameyasema hayo katika mahojiano maalum na Redio Ultimate FM ya Kumasi, Ghana.
“Ngono kupita kiasi” ndiyo sababu aliyoitaja kupunguza nguvu za wachezaji Ghana.
Kwa mujibu wa kocha huyo mkongwe, asilimia kubwa ya wachezaji wa siku hizi wanaondolewa njiani kwa urahisi na hawana uwezo wa kucheza muda wote wa mchezo kwa sababu hawalali vizuri na hawana mazoezi ya kutosha.
“Wachezaji wengi wa leo hawawezi kucheza dakika 90, kwa sababu wanachoka haraka. Na unajua kwa nini? Kwa sababu hawalali kiasi cha kutosha na hawapati mazoezi ya kutosha na wanafanya ngono sana.”
“Kuna wasichana wazuri wadogo Ghana Ghana na hawawezi kuwaacha peke yao,” amesema kocha Malik Jabir akizungumza na Ultimate FM na kushauri;
“Kuna
wakati wa hayo mambo, na wakati wa soka. Ukiyachanganya hayo mambo
mawili, huwezi kufika juu,".
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni