WATANI
wa jadi, Simba na Yanga wamegawana pointi baada ya kutoa sare ya
kufungana bao 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi
unazidi kupandisha kileleni Simba SC ikifikisha pointi 17, baada ya
kucheza mechi saba, wakati Yanga inatimiza pointi 11 baada ya kucheza
mechi sita.
Katika
mchezo wa leo Yanga walitangulia kwa bao la Mrundi, Amissi Joselyn
Tambwe kabla ya mzalendo, Shizza Ramadhani Kichuya kuisawazishia Simba
SC iliyocheza pungufu kwa muda mrefu baada ya Jonas Mkude kutolewa kwa
kadi nyekundu kipindi cha kwanza.
Tambwe
alifunga bao lake dakika ya 26, akimalizia pasi ndefu ya beki Mbuyu
Twite na kugeuka mbele ya beki wa Simba, Novat Lufunga kabla ya kufumua
shuti lililomshinda kipa Vincent Angban.
Bao
hilo lilizua kizaazaa, wachezaji wa Simba wakimvaa refa Martin Saanya
wakidai mfungaji, Tambwe aliushika mpira kabla ya kufunga.
Katika
vurugu hizo, Saanya akamtoa kwa kadi nyekundu Nahodha wa Simba SC,
Jonas Mkude dakika ya 29 kwa sababu ndiye aliyekuwa mstari wa mbele.
Na
mchezo ukasimama kwa takriban dakika tano baada ya mashabiki wa Simba
kuanza kufanya vurugu waking’oa viti na kutupa uwanjani.
Polisi walitumia milipuko kuwatuliza mashabiki hao na mchezo ukaendelea.
Kipindi
cha pili, Simba SC walibadlika pamoja na kucheza nguvu wakafanikiwa
kupata bao la kusawazisha lililofungwa na winga Shizza Kichuyaa dakika
ya 87 baada ya kona aliyochonga kuingia moja kwa moja nyavuni.
Kikosi
cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa 'Barthez',Juma Abdul,Mwinyi Hajji,
Kevin Yondan/Andrew Vincent dk46, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Juma
Mahadhi/Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Amisi Tambwe, Donald Ngoma na
Deus Kaseke/Haruna Niyonzima.
Simba
SC; Vincent Angban, Janvier Besala Bokungu, Mohammed Hussein
'Tshabalala', Novart Lufunga/Juuko, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shizza
Kichuya, Muzamil Yassim, Laudit Mavugo/Blagnon, Ibrahim Hajib/Mohamed
‘Mo’ Ibrahim na Mwinyi Kazimoto.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Jumamosi, 1 Oktoba 2016
SIMBA PUNGUFU WAIKAZIA YANGA KAMILI, VITI VYANG'OLEWA, MABOMU YAPIGWA
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni