Baada ya kutoka sare katika mchezo uliopita klabu ya kongwe ya Yanga leo imerudisha tena makali yake baada ya kuifumua klabu ya Majimaji ya Songea mabao matatu kwa bila.
Yanga walipata penati katika dakika ya 13 ya mchezo na Simon msuva ndiye aliyekuwa mpigaji, Msuva aliweka kimiani mpira huo na mwamuzi alikataa na kutaka penati irudiwe na msuva tena akaweka kwa mara ya pili kimiani lakini mwamuzi Emmanuel Mwandebwa alikataa kwa mara ya pili.
Hatimae mara ya tatu Msuva alikosa penati na Deus Kaseke alimalizia mpira na kufanya matokeo kuwa 1-0 mpaka mapumziko.
Kikosi cha Yanga kilikuwa; Ally Mustapha ‘Barthez’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Vincent Andrew/Kevin Yondan dk85, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Thabani Kamusoko, Simon Msuva/Yussuf Mhilu dk88, Obrey Chirwa/Juma Mahadhi dk46, Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Deus Kaseke.
Maji Maji: Agathon Anthony, Bahati Yussuf, Suleiman Kibuta, Hamad Kibopile, Ernest Raphael, Lulanga Mapunda, Alex Kondo, Mfanyeje Yusuph, Hassan Hamisi, Marcel Bonivanture na Paul Mahona/Peter Mapunda dk55.
Kipindi cha pili Hans van der Pluijm alimtoa Obrey Chirwa na nafasi yake kuchukuliwa na Juma Mahadhi aliyekwenda kupika mabao Mawili yaliofungwa na mfungaji bora wa msimu uliopita Amiss Tambwe katika dakika ya 78 na 85.
Wakati huo pale Azam FC wameondoka jijini Mbeya kibabe baada kujizolea pointi sita kutokana na ushindi walioupata dhidi ya Prisons na Mbeya City iliyokubali kipigo cha mabao 2-1 kwenye dimba la Sokoine leo.
Kiungo Hamis Mcha alikuwa wa kwanza kuwainua vitini mashabiki wachache wa Azam waliohudhuria mchezo huo kwa bao safi la dakika ya 10 kwa shuti kali alilopiga akiwa nje ya 18.
Dakika mbili baadae City walipata penati baada ya Michael Balou kumfanyia madhambi Joseph Mahundi, penati hiyo ilikwamishwa wavuni na Raphael Daud.
Dakika ya 45 Ya Thomas Renardo alimalizia kiufundi krosi ya Mcha na kuipatia Azam bao la pili na la ushindi katika mchezo huo uliokuwa mgumu kwa pande zote.
Kipindi cha pili City walitawala mchezo lakini hawakufanikiwa kusawazisha bao hilo hivyo kukubali kipigo cha nyumbani.
MATOKEO YOTE 2016-09-10;
FT | MWADUI FC | 2 | : | 2 | STAND UNITED |
FT | MBEYA CITY | 1 | : | 2 | Azam FC |
FT | NDANDA FC | 0 | : | 0 | KAGERA SUGAR |
FT | YANGA | 3 | : | 0 | MAJIMAJI |
FT | RUVU SHOOTING | 1 | : | 0 | JKT RUVU |
MICHEZO YA KESHO-2016-09-11
16:00 | SIMBA SC | Vs | MTIBWA SUGAR |
16:00 | T.PRISONS | Vs | TOTO AFRICANS |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni