Habari ni kwamba Shirikisho la soka nchini TFF wametoa tamko mchana huu kwamba mechi ya Azam na Simba itapigwa siku ile ile kama ratiba ilivyo pangwa hapo awali.
Mwanzo zilisikika tetesi katika vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii kwamba mechi imehairishwa mpaka Septemba 21,Lakini Afisa habari wa Tff bwana Alfred Lucas alieleza kwamba mechi ipo na itachezwa Septemba 17 Jumamosi hii.
.
Pia Alfred Lucas ameeleza kuhusu swala la Klabu ya Azam kutaka mechi hii ichezwe katika uwanja wao wa Nyumbani alisema kwamba waliweza kukaa na klabu ya Azam na kushauriana na hatimaye walifikia muafka na Azam wamekubali mchezo huu uchezwe katika dimba la Uhuru kutoka katika ule uwanja wa Chamanzi.
“Azam FC wameielewa hoja ya TFF na mchezo wao dhidi ya Simba utafanyika katika uwanja wa Uhuru Septemba 17 kama kawaida saa 10 ratiba haijabadilika, makubaliano ambayo yamefikiwa na CEO wa Azam FC Saad Kawemba na katibu mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa”
STORI YA PILI;
Nahodha wa Chelsea John Terry atakuwa nje kwa siku kumi bada ya kupata majeraga kwenye mguu wake wakati wa mchezo wa Ligi ya England mwishoni mwa wiki dhidi ya Swansea ambapo walitoka sare ya mabao 2-2, mchezo uliopigwa Uwanja wa Liberty.
Majibu ya vipimo alivyofanyiwa jana yanaonesha kuwa ataukosa mchezo wa Ijumaa dhidi ya Liverpool utakaopigwa Stamford Bridge.
Baada ya mchezo wa Jumapili meneja Antonio Conte: “Sifahamu kiasi gani amepata maumivu lakini kesho (Jumatatu) tutapata kujua kuhusu ankle yake. Lakini ni mpiganaji yule. Sina shaka naye worried.”
Kukosekana kwa John Terry ni ni nafasi kwa beki wa kimataifa wa Brazil David Luiz, ambaye amerejea Stamford Bridge akitokea Paris St-Germain kwenye dirisha la kiangazi lililofngwa hivi karibuni.
STORI YA TATU;
Meneja
wa Arsenal Arsenal Wenger amesema kwamba kukosekana kwa Zlatan
Ibrahimovic kwenye klabu ya Paris Saint-Germain ni pigo kubwa kwani
wamepoteza mtu ambaye alikuwa zaidi ya mchezaji.
Ibrahimovic
amefanikiwa kujitengenezea historia yake PSG baada ya kuweka rekodi ya
kuwa mfungaji bora wa muda wote kwenye klabu hiyo yenye maskani yake
Parc des Princes.
Msweden huyo aliondoka PSG mwishoni mwa msimu uliopita na kujiunga na Manchester United.
Wenger amesema: "Wataendelea kuwa timu itakayotawala soka la Ufaransa lakini wamepoteza zaidi ya mchezaji.
"Alikuwa
ni kiongozi, nahodha, mwenye kukubali kutokana na mtazamo wake chanya
usiopimika klabuni, sasa unapompoteza mchezaji wa aina hiyo ni pigo
kubwa.
"Kwa sasa pia wamebadili meneja, hivyo wanajaribu kuendana na mfumo mpya."
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni