RAIS mpya wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA, Aleksander Ceferin amebainisa logo mpya itakayotumika katika michuano ya Ulaya 2020 katika sherehe zilizofanyika jijini London mapema leo.
Logo hiyo inaonekana ikiwa katika rangi tofauti huku picha za mfano wa mashabiki wakiwa pande zote kulizunguka kombe la michuano hiyo ikiwakilisha uhusiano wa nchi 13 wenyeji.
Michuano hiyo ya 2020 itafanyika katika miji 13 tofauti barani Ulaya ili kusheherekea miaka 60 toka kuanzishwa kwake, huku nusu fainali na fainali zikitarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Wembley nchini Uingereza.
Akizungumza katika sherehe hizo, Ceferin amesema UEFA inataka michuano ya 2020 kuwa ya kweli kushangilia mafanikio ya mchezo huo unaopendwa na kutukuzwa. Mechi zingine za michuano hiyo pia zitachezwa katika nchi za Azerbaijan, Ubelgiji, Denmark, Ujerumani, Hungary, Ireland, Italia, Uholanzi, Romania, Urusi, Scotland na Hispania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni