TIMU
ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imeshindwa
kukata tiketi ya Fainali za Afrika mwakani Madagascar baada ya kufungwa
1-0 na wenyeji Kongo - Brazzaville jioni jii Uwanja wa Kumbukumbu ya
Alphonse Massamba-Debat mjini Brazaville katika mchezo wa marudiano
hatua ya mwisho ya mchujo.
Kwa
matokeo hayo, Serengeti Boys inatolewa kwa bao la ugenini baada ya sare
ya jumla ya 3-3, kufuatia kushinda 3-2 katika mechi ya kwanza wiki
mbili zilizopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji
wa Serengeti Boys iliyo chini Mkurugenzi wa Ufundi, Mdenmark Kim
Poulsen, Kocha Mkuu, Bakari Shime na Kocha wa makipa na Muharami
Mohammed ‘Shilton’ wapo kwenye huzuni kubwa baada ya matokeo hayo mjini
Brazzaville.
Hii
inakuwa mara ya pili Serengeti Boys kuikosa kosa tiketi ya fainali za
Afrika baada ya mwaka 2005 kufuzu fainali za Gambia, kwa kuzitoa Rwanda,
Zambia na Zimbabawe, lakini ikaenguliwa kwa kashfa ya kumtumia mchezaji
aliyezidi umri, Nurdin Bakari aliyekuwa anachezea Simba SC wakati huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni