JINSI MOURINHO ALIVYOCHAKWAZWA TWITTER BAADA YA KUPAKI BASI JANA;
KILICHOANDIKWA TWITTER JUU YA POGBA BAADA YA MCHEZO DHIDI YA LIVERPOOL JANA???
SAVE YA DE GEA YAWAKIVUTIO MCHEZO DHIDI YA LIVERPOOL;

Mchezo kati ya Liverpool dhidi ya Manchester United ulichagizwa na
kazi ya ziada iliyofanywa na golikipa wa Manchester United mhispania
David De Gea kuokoa mchomo wa fundi wa kibrazil Phil Coutinho.

Dakika ya pili ya mchezo huo, De Geal aliiokoa timu yake kwa kuokoa
mpira uliopigwa na Emre Can lakini kazi liyoifanya kuzuia kazi nzuri
iliyofanywa na Coutinho ndiyo ilikuwa save ya maana katika mchezo huo.
Coutinho alijitahidi kupiga mpira kwa ustadi kwa kutumia mguu wake wa
kulia nje kidogo ya box na mashabiki wengi waliamini mpira huo ulikuwa
unatinga kambani.
Lakini ubora wa De Gea uliiweka United salama ikiwa ni miongoni mwa
changamoto nyingi ambazo amefanikiwa kufaulu kwenye maisha yake ya soka
akiwa Manchester United.
Tukio hilo lilionekana kuwa ndio lililowavutia mashabiki wengi walioshuhudia mchezo huo kuliko matukio mengine yoyote.


ENDAPO MANCHESTER UNITED WATACHUKUA UBINGWA MSIMU HUU BASI WATAWEKA REKODI YA TIMU AMBAYO KATIKA MICHEZO NANE YA MWANZO WALIKUWA NAFASI YA SABA

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni