MSHAMBULIAJI nyota wa
Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesema hoteli yake mpya aliyozindua ni
sehemu ya maandalizi yake ya maisha baada ya soka, ingawa mwenyewe
amedai anaweza kucheza katika kipindi cha miaka 10 ijayo.
Ronaldo
alisafiri moja kwa moja kuelekea jijini Lisbon baada ya sare ya bao 1-1
waliyopata Madrid dhidi ya Eibar jana mchana, ambapo jioni ya siku hiyo
alifungua rasmi hoteli yake inayoitwa Pestana CR7 Lisboa.
Akizunguza
katika uzinduzi huo, Ronaldo amesema maisha sio soka peke yake na ingawa
ni mchezo anaoupenda lakini lazima afikirikie maisha yake baada ya
soka.
Hoteli hiyo kubwa ya kifahari itakuwa na vyumba vinavyoanzia bei
ya euro 200 mpaka 1,200 kulingana na uwezo wageni watakaokuwa
wakimiminika katika hoteli hiyo ya vyumba 82 iliyopo jijini Lisbon.
Taarifa zinadai kuwa Ronaldo na mshirika wake Pestana wamewekeza kiasi
cha euro milioni 15 katika hoteli huku wakipanga kufungia zingine mbili
katika jiji la Madrid na New York.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni