KLABU ya Swansea City
imemtimua meneja wake Francesco Guidolin na nafasi kuchukuliwa na kocha
wa zamani wa timu ya taifa ya Marekani Bob Bradley.
Swansea hawajashinda
mechi yeyote ya Ligi Kuu toka kuanza kwa msimu na sasa wanashika nafasi
ya 17 katika msimamo.
Bradley ambaye pia amewahi kuzifundisha Misri na
klabu ya Stabaek ya Norway, anaiacha timu ya Le Havre inayoshiriki ligi
daraja la pili Ufaransa na kwenda kuchukua nafasi ya Guidolin
aliyeteuliwa Januari mwaka huu.
Viongozi wa klabu hiyo wanadaiwa
kuzungumza na makocha kadhaa kwa ajili ya nafasi hiyo akiwemo nahodha wa
zamani wa kimataifa wa Wales Ryan Giggs.
Kibarua cha kwanza cha Bradley
mwenye umri wa miaka 58, kitakuwa kusimamia mchezo dhidi ya Arsenal
Octoba 15 mwaka huu baada ya mapumziko kupisha mechi za kimataifa
kumalizika.
KLABU ya Aston Villa
imemtimua meneja wake Roberto di Matteo baada ya kudumu katika kazi hiyo
kwa siku 124 pekee.
Villa kwasasa wanatafuta meneja mpya ambaye atakuwa
wa nne katika kipindi cha mwaka mmoja baada ya kumtimua Muitaliano huyo
ambaye ameshinda mechi moja kati ya 11 za ligi ya ubingwa
alizosimamia.
Di Matteo mwenye umri wa miaka 46 ambaye pia amewahi
kuinoa Chelsea, aliteuliwa muda mfupi baada ya mfanyabiashara Dr Tony
Xia wa China kuinunua klabu hiyo Juni 2.
Msaidizi wa Di Matteo, Steve
Clarke ndio amepewa mikoba ya muda kuiongoza klabu hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni