STORI YA KWANZA;
Timu
ya Taifa ya Vijana ya Tanzania chini ya miaka 17 'Serengeti Boys' juzi
walipoteza nafasi ya kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa
Vijana Chini ya miaka 17 baada ya kufungwa bao 1-0 na Congo Brazzaville
Serengeti
Boys wamejikuta wakitupwa nje kwa faida ya goli la ugenini kufuatia
mchezo wa awali uliochezwa Uwanja wa Taifa kushinda kwa mabao 3-2, hivyo
Congo kuwa na wastani mzuri wa magoli ya ugenini.
Baada ya hali hiyo, Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi ameonesha kusikitishwa na matokeao hayo huku akielezea namna vijana pia walivyoumizwa mpaka kufikia hatua ya kulia punde tu baada ya mchezo kumalizika.
Malinzi
amesema: "Poleni kwa matokeo ya juzi. Baada ya mechi vijana walilia
sana. Imeumiza lakini ndio mpira.Timu itatua jumanne usiku sa3 kwa
Rwanda air.
Jumatano tutakula nao chakula cha mchana na kuwaeleza nini
matarajio yetu kwao. Na kikubwa watajulishwa kwamba wao sasa ndio
Ngorongoro Heroes ya 2019.
Taratibu tutajenga Taifa stars ya 2021 kwa
kuwashirikisha kwa karibu vijana hawa. Kikubwa ni sisi viongozi kutokaa
nao mbali na kuzidi kuwapatia mechi hasa za kimataifa. Ni muhimu wakue
pamoja."
STORI YA PILI;
WACHEZAJI WANAOUNDA KIKOSI BORA CHA EPL BAADA YA MECHI ZA WIKIENDI
KIKOSI KIBOVU CHA EPL BAADA YA MICHEZO YA WIKIENDI HII
STORI YA TATU;
VIDEO- TUKIO LA RONALDO KUGEUKA BALL BOY?
Cristiano Ronaldo ni mtu anayependa sana wakati mwingine kutumia muda wake wa ziada kufanya mamabo yanayoweza kuwafurahisha kupelekea ku-refresh akili yake.
Amewahi
kufanya matukio mbalimbali ya kufurahisha jamii kama lile la kuvaa
'mask' na kucheza mpira katikati ya jiji la Madrid na mengine mengi tu.
Sasa
kuna hili tukio jingin ni hili la kugeuka kuwa “ball boy”, wa timu ya
watoto ambayo mwanaye alikuwa miongoni mwa wachezaji kwenye timu hiyo.
Wakati mpira ulipokuwa ukitoka nje ya uwanja, basi Ronaldo alikuwa akibeba jukumu la kufuata mpira na kurudisha uwanjani.
VIDEO;
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni