TAARIFA YA KWANZA;
YANGA SC imeomba kutumia Uwanja wa Amaan, Zanzibar kwa mechi zake mbalimbali za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Taarifa
ya Kaimu Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit imesema kwamba hatua hiyo
inafuatia Serikali kuizuia klabu hiyo pamoja na mahasimu wao, Simba SC
kutumia Uwanja wa Taifa.
Yanga
imeiandikia barua Wizara ya Habari Utakii na Michezo Zanzibar kuomba
kuhamia Uwanja wa Amaan, baada ya kufungiwa kwa Uwanja wa Taifa.
Juzi, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye alitangaza kuzuia Simba na Yanga kutumia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya vurugu zilizosababisha uharibifu Jumamosi katika mechi baina ya watani hao wa jadi.
Mashabiki wa Simba Jumamosi walifanya vurugu Uwanja wa Taifa baada ya Yanga kupata bao la kuongoza lililofungwa na mshambuliaji Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Tambwe alifunga bao lake dakika ya 26, akimalizia pasi ndefu ya beki Mbuyu Twite na kugeuka mbele ya beki wa Simba, Novat Lufunga kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa Vincent Angban.
Bao hilo lilizua kizaazaa, wachezaji wa Simba wakimvaa refa Martin Saanya wakidai mfungaji, Tambwe aliushika mpira kabla ya kufunga.
Katika vurugu hizo, Saanya alimtoa kwa kadi nyekundu Nahodha wa Simba SC, Jonas Mkude dakika ya 29 kwa sababu ndiye aliyekuwa mstari wa mbele.
Na mchezo ukasimama kwa takriban dakika tano baada ya mashabiki wa Simba kuanza kufanya vurugu waking’oa viti na kutupa uwanjani.
Polisi walitumia milipuko ya gesi za kutoa machozi kuwatuliza mashabiki hao na mchezo ukaendelea hadi Simba SC wakasawazisha dakika ya 87 kwa bao la Shizza Kichuya.
Nape alisema kwamba mbali na uvunjwaji wa viti, pia mageti mawili ya kuingilia, moja la upande wa Yanga na lingine wa Simba yamevunjwa.
Awali ya hapo, Kaimu Mkurugenzi wa Michezo, Alex Nkenyenge alisema kwamba zaidi ya viti 1781 vilivunjwa juzi katika mchezo ambao kati ya Sh. Milioni 350 na 400 zikikusanywa katika viingilio vya mashabiki waliingia kwa tiketi za Elektroniki.
JE, KWA MUJIBU WA KANUNI ZA TFF YANGA WATARUHUSIWA KWENDA ZANZIBAR KUTUMIA UWANJA WA AMAAN? SOMA HAPA
TAARIFA YA PILI;
Rais wa Fifa Gianni Infantino
ameshauri kuongezwa wa timu zinazoshiriki kombe la dunia na kufikia 48
zaidi ya ahadi yake aliyoitoa wakati akiwania nafasi hiyo kuwa
atafikisha timu 40.
Kisha kubaki 32 zitakazoendelea katika makundi baada ya hatua ya mtoano kukamilika.
Infantino anasema kuwa mapendekezo hayo yatapelekwa katika bodi ya Fifa Januari.
''Haya ni mawazo ya kupata suluhisho la uhahika, tutayajadili mwezi huu na kufahamu nini cha kufanya mwaka 2017,'' alisema Infantino mwenye miaka 46.
Infantino aliingia madarakani kuliongoza shirikisho hilo la Fifa mwezi Februari baada ya kujiuzulu kwa Sepp Blatter.
TAARIFA YA TATU;
BALOTELLI AMZUNGUMZIA KLOPP;
Mario
Balotelli amefichua kwamba hakuwa na uhusiano wowote na Jurgen Klopp,
ambaye alimwambia mchezaji huyo kuondoka Liverpool kwa mkopo.
Muitaliano
huyo alisajiliwa na Brendan Rodgers mwaka 2015 kutoka AC Milan, lakini
alishindwa kabisa kuonesha makali yake kabl ya kurudi tena AC Milan kwa
mkopo.
Kwa
sasa anakipiga kunako klabu ya Nice, ambapo tayari ameshafunga mabao
sita kwenye michezo mitano baada ya kuondoka Liverpool bure kwenye
dirisha la usajili la majira ya kiangazi.
Na
sasa Balotell amefichua kwa kusema kwamba hapakuwa na uwezekano wowote
kwake kurudi Anfield kutokana na uhusiano usioridhisha kati yake na
Klopp.
"Klopp?
Simjui mimi huyo mtu," Balotelli aliiambia Sky Sport Italia.
"Aliniambia tu niondoke Liverpool kwa mkopo na baadaye nikarejea
kumwambia: 'Asante sana, na kwaheri.'"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni